siku mbili baada ya kuzusha taflani kufuatia sakata la uhamisho kutoka timu yake ya zamani ya Azm Fc, nyota wa klabu ya Simba Mrisho ngasa ameanza mazoezi rasmi asubihi ya leo mara baada ya kukamilika kwa taratibu za usajili wake mapema jana.
Akizungumza na teentz.com muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi hayo Ngasa amedokeza kuwa anataka kufanya mambo makubwa akiwa na timu yake hiyo mpya na amewaomba mashabiki wa Simba kumuamini na kumpa ushirikianao.
"sina kingine, nataka kufanya makubwa nikiwa na timu yangu mpya naomba mashabiki waniamini na kunipa ushirikiano" alisema
Ngassa amejiunga na Simba na kukabiziwa jezi namaba 16 sambamba na ndinga ya kisasa aina ya Verossa huku akilamba shavu la kuvuta mshahara wa shilingi za kibongo Milioni 2 kwa Mwezi
STORI NA DISMAS TEN 0718489260.
No comments:
Post a Comment