ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 2, 2012

Sijazuia Kagoda kushitakiwa


Aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali.


Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa suala la ubadhirifu wa Sh. bilioni 40 zinazodaiwa kuchotwa na kampuni ya Kagoda Agriculture kati ya Sh. bilioni 133 za akaunti ya malipo ya nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) halipo mikononi mwake.

Akijibu maswali ya wahariri wa vyombo vya habari  Ikulu jana jijini Dar es Salaam alisema suala la uchunguzi wa upotevu wa fedha hizo upo mikononi mwa vyombo husika.

“Sisi hatuna kizuizi. Vyombo vya uchunguzi vinahusika,” alisema Rais Kiwete bila kuingia kwa udani zaidi kuhusu suala hilo.



Kagoda ni miongoni mwa kampuni zilizojinufaisha na wizi wa fedha za Epa ikijichotea Sh. bilioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa, lakini hadi leo tangu sakata hilo lifumuke mwaka 2008 na kusababusha baadhi ya watu kufikishwa mahakamani, mmiliki wake anadaiwa kuwa hajukikani.

Sakata la Kagoda lilisanisha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kuandika barua kwa wakaguzi wa Deloitte & Touche akisema kuwa fedha iliyochota BoT zilikuwa ni kwa ajili ya masula ya usalama, lakini baadaye akafuta barua hiyo ana kueleza kuwa alikuwa amepotishwa na aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali.
Katika mkutano huo pia Rais Kikwete alijibu swali la kuhusu watuhumiwa wa rada kutochukuliwa hatua, alisema walioanzisha suala hilo ni Taasisi ya Kupambana na Makosa Makubwa ya Udanganyifu ya Uingereza (SFO).

Alisema aliletewa ujumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza na maofisa wa SFO waliomba kuwahi baadhi ya watu nchini, hata hivyo hakuwataja, na aliwaruhusu.

Rais alisema baada ya kuwahoji maofisa hao, SFO walirudi Uingereza na kukaa kwa muda mrefu pasipo taarifa yoyote, lakini walishangaa kusikia kwamba kampuni iliyokuwa imetuhumiwa kwa rushwa ya BAE System ikikiri mahakamani kwamba ikikiri mahakamani kwamba ilifanya makosa ya kutoweka kumbukumbu za kiuhasibu tu, hivyo kuamua kulipa fidia kwa nchi iliyokuwa imefanya nazo biashara ikwamo Tanzania, Saudi Arabia na Marekani.

“Sasa aliyekuwa anatuhumiwa kwa rushwa amekataa kuhusika na rushwa, amekiri kosa la kuuhasibu la kuweka hesabu vibaya, hapa unamshitaki vipi mtu wakati kampuni yenyewe (BAE) haipo,” alihoji Rais Kikwete na kuongeza:

“Hata jaji (wa Kiingereza) aliyeamua kesi hiyo hakufurahishwa na utaratibu uliotumika.”
Ingawa Rais hakutaja ofisa yeyote wa serikali ambao aliridhia wahojiwe, walihojiwa na SFO wakati huo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, wakati huo akiwa Waziri wa Miundombinu na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk. Idris Rashid.

Wakati wa mchakato wa kununua rada, Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Rashidi alikuwa Gavana wa BoT.

Chenge aligundulika kuwa na kiasi cha Dola milioni moja za Marekani katika akaunti yake visiwa vya Jersey, taarifa ambazo hakuwa amezitaja kwenye fomu za kutangaza mali na madeni kwa Sekretariati ya maadili ya viongozi.

Hata hivyo amekanusha kuhusika na rushwa katika ununuzi wa rada.

Tanzania iliuziwa rada ya bei mbaya ya Sh. bilioni 70 wakati huo na baada ya sekeseke kubwa BAE walamua kuirejeshea Tanzania Sh. bilioni 72 za rada fedha  zilizobatizwa jina la chenji ya rada, ilahli watu wengine wakisema si chenji ila ni rushwa ya rada.


 
CHANZO: NIPASHE

2 comments:

Anonymous said...

Tunashangazwa sana kuona viongozi wengi tu kwa mfano Andrew Chenge na Edward Lowasa na wengineo wengi bado wapo madarakani katika serikali yetu na wakati wanajulikana kuwa ni mafisadi!Wanaifilisi Tanzania na hawana huruma na nchi yetu!Sifahamu kwanini serikali yetu bado inawakumbatia watu kama hao!

lcs said...

Na kama hizi biloni 72 ni fedha za walipa kodi ,kwanini serikali inalazimishwa kununulia vitabu sehemu ya fedha hizo toka Ulaya. au huu ni ufisadi mwingine kwani vitabu huko Ulaya na marekani vinatolewa kama msaada na ikitiliwa maanani vitabu vingi vinakuwa vimeshapitwa na wakati / outdated books