|
Sisi
ni watu wa kujali jamii bwana... Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey
Nyange 'Kaburu' (katikati) akiwa pamoja na nahodha wa timu hiyo, Juma
Kaseja (kulia) na beki Juma Nyosso (kushoto) wakibeba vyandarua na
zawadi nyingine kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa wakati walipotembelea
hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo. Picha: Sanula
Athanas |
|
Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akiwa katika eneo la hospitali ya Mwananyamala. Picha: Sanula Athanas |
|
Chu chu chuuuuu.... tototoooooooo |
|
Mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha usajili, Salim Kinje pia alikuwepo Mwananyamala Hospital. |
|
Lengo
letu ni kusaidia jamii hivi kila mara... Kaburu (kulia) akitoa mawili
matatu wakati Simba ilipotembelea wagonjwa na kutoa zawadi leo. |
|
Mnaonaje hali ya hapa hospitali? |
|
Juma K. Juma akitoa chandarua kwa mgonjwa |
|
Kaburu akiongoza msafara |
|
Hii ndio Coaster yetu lakini basi kubwa la kisasa linakuja Agosti 15 |
|
Ezekiel Kamwaga akijiandaa kumwaga vyandarua hospitalini Mwananyamala leo |
|
Leo sio mwisho, tutakuja tena na tena... Kaburu akizungumza na akina mama hospitalini Mwananyamala |
VIONGOZI, wachezaji na wazee mbalimbali
wa mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wamefanya tukio la
kihistoria leo baada ya kutembelea wagonjwa kwenye Hospitali ya
Mwanaymala jijini Dar es Salaam na kugawa misaada mbalimbali.
Tukio
hilo nadra kuonekana likifanywa na klabu za soka nchini limeelezewa na
uongozi wa Simba kuwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku maalum ya
kila mwaka ya klabu hiyo ya 'Simba Day'.
Makamu Mwenyekiti wa
klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' ndiye aliyeongoza msafara huo huku
kwa upande wa wachezaji, kipa na nahodha Juma Kaseja ni miongoni mwa
nyota walioshiriki kukabidhi misaada hiyo, akiambatana na nyota wenzake
kadhaa wakiwamo Juma Said Nyosso, Kigi Makassy na kiungo aliyesajiliwa
msimu huu kutoka Kenya, Salim Kinje.
Akizungumza hospitalini
hapo, Kaburu alisema kuwa wamewatembelea wagonjwa na kuwapa misaada kwa
vile klabu yao ni sehemu ya jamii na hivyo wanapaswa kurejesha kidogo
wanachokipata kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum.
Akaongeza
kuwa mbali na kutembelea wagonjwa, pia watatembelea baadhi ya vituo vya
watoto yatima na kuwapelekea misaada mbalimbali.
Baadaye, msafara
huo wa Simba uliowatembelea wagonjwa waliolazwa katika wodi ya akina
mama wajawazito na pia ya watoto waligawa vitu mbalimbali kama
vyandarua, maji na sabuni.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk.
Sophinias Ngonyani, aliwashukuru viongozi na wachezaji wa Simba kwa
hatua yao ya kuwatembelea na kugawa misaada kwa wagonjwa; huku pia
akiziasa klabu za soka na wanamichezo wengine kuiga moyo huo.
MTOTO APEWA JINA 'JUMA KASEJA'
Katika tukio mojawapo la kusisimua
hospitalini hapo, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rose Joseph
alisema kuwa amefurahi sana kuwaona 'live' wachezaji wa timu
anayoishabikia ya Simba an kwamba, ameamua kumpa jina la 'Juma Kaseja'
mtoto wake aliyemzaa leo asubuhi kwa vile alipata bahati ya kubebwa na
kipa huyo nyota wa 'Wekundu wa Msimbazi' na timu ya taifa, Taifa Stars.
“Nimefurahi sana kumuona Kaseja akimbeba mwanangu,” alisema Rose.
No comments:
Post a Comment