ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 26, 2012

UFUNGUZI WA TAWI LA CCM DMV FUNIKA BOVU

 MH. Abdulrahman Kinana akiingia ukumbini uku akiongozana na viongozi wa tawi la CCM hapa DC.


 MH. Abdulrahman Kinana akipiga makofi huku akiingia ukumbuni hapo tayari kwa ufunguzi wa tawi la CCM, watu wengi walijitokeza katika ufunguzi huo na kujipatia kadi za chama chao tawala cha CCM.
 Picha ya pamoja ya viongozi wote wa matawi mengine ya CCM kutoka sehemu tofauti za nje ya DC kama Minnesota kiongozi wake alikuwepo, North Carolina, New York na Texas.
 Meza kuu na ya viongozi wakiwa wametulia kabisa wakisikiliza risala liyokuwa inasomwa ukumbuni hapo
 Loveness mwenyeketi wa tawi la CCM, DMV akiongea maneno mawili matatu kabla ya kumkaribisha mgeni rasm katikia shughuri hizo za ufunguzi wa tawi la CCM.
Watu wengi sana walijitokeza kati ufunguzi huo kama unavyo ona katika picha
 MH. Abdulrahman Kinana akiongea baada ya kukaribishwa na mwenyekiti wa tawi la CCM, DMV Loveness.
Wakereketwa wa CCM wakiwa ukumbini
Baadhi ya Viongozi na wakereketwa wa CCM wakipata picha ya pamoja na Mhe. Abdulrahman Kinana kwenye ufunguzi wa Tawi la CCM, DMV.
Wakereketwa wakisakata Rhumba
Mume wa Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Bwna Shariff Maajar (wapili toka kushoto) katika picha ya pamoja na Salma JJ (kushoto) Missy Temeke na Miss Kigoma kutoka Columbus, Ohio (kulia)
Kwa picha zaidi bofya ready more.





















13 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli nimeamini ule usemi,usisikie la kuambiwa mpaka uone mwenyewe..kumbe fitna zote zilikuwa bure kabisa..mimi sio ccm..nimekubali jama a wamejipanga...very class affair..

Anonymous said...

CCM MMEFUNIKA....this is what i call uzalendo, siyo ule ugomvi wa kule chama pinzani

Anonymous said...

"penye uzia penyeza rupia", wengi wao wako na sababu zao tofauti sio mapenzi ya kweli na ccm, zaidi nasema wanaangalia maslahi na sio mapenzi na ccm, kuna watu hapo hakuna wasijua kuwa walidhalilishwa na ccm na wakawa namba one kuichukia ccm, leo wanaonekana na mashati ya kijani, wanajua ukitaka ulaji nenda ccm. CCM OYEE, ULAJI OYEE

Anonymous said...

huyo anaechukua kadi hapo ni kijana wa kirundi anjilinda familia yake isifukuzwe TZ

Anonymous said...

Hizo ni chuki na utenganishi ndani ya jamii yetu.
Kwanza wewe unayesema kuwa huyo ni Mrundi, na wewe ni nani kama sio Mganda au Mkenya au Mmalawi, tukianza kusema hivi tutafika wapi? Ukabila na udini utafuata. Hizo zote ni kauli za watu wasio elimika na wachochezi. Elimu ni muhimu katika maisha sio kuwa ulaya basi wewe unaakili maarifa, Jielimishe na upate kupevuka kiakili.
Pili, wewe unayesema kuwa CCM ni ulaji,Wewe ni T-can hizo zote ni kauli za akili finyu, Kutoelimika ni kubaya sana, kwani wewe unaona vyama vya upinzani sio ulaji. Kwa kukuelimisha angalia wote upinzani wanatafuta ulaji wapi wapate ulaji. Na njia ya kupata ulaji ni kukutumia wewe mwenyeakili finyu yakutoweza kutafakari ujumbe/maneno wanayo waambieni. Nawatuwengi wako huko upinzani ni tamaa ya vyeo na makulaji. wengine mnategemea kupewa ubalozi na wengine manategemea kupewa madaraka. Sasa angalia, mtu kama wewe upewe madaraka utafanya nini na kama sio kutenganisha wananchi? Elimu Dunia finyu, Elimu Ahera bure, sasa utafanya nini. Acheni chuki, fitna na majungu.

Anonymous said...

Hata sikutegemea ingekua hivi!! kweli wanachama wa ccm ni watu na akili zao, achana kabisa na fitna za watu kwenya mablog zisizo na maana.

Anonymous said...

wewe unayeongelea mabaya ya CCM eti walizalilishwa na CCM?!!mazuri yapi uliyofanyiwa na hivyo vyama vingine?!!!wewe CCM imekusomesha the door is open get the ....here!!

Anonymous said...

Hao wote unaowaona hapo ni kwa sababu walidanganywa kuwa hawataingia ndani ya ukumbi mpaka wawe na kadi na wengine wakavaa na kama unavyoona kwa kuwa waliambiwa Diamond atakuwepo na matokeo yake hakutokea hata hivyo humo ukumbini kulikuwa na wa-Zaire/Congo na raia wa hapa USA pia meza zilizotumika ni 12 tu sasa hebu fikiria kila meza inachukua watu wangapi..!!!??(Angalia picha ya 17 kutokea chini ndio ujue kuwa watu wapo humu MAGAMBANI kimaslahi zaidi na ukitaka kujua zaidi angalia picha zote kwa umakini zinajieleza vizuri mnoooo utanielewa ninachomaanisha...MKATA MKAA JANGWANI

Anonymous said...

Hapo hakuna cha uzalendo wala nini maana watu walikubali kununua kadi ili iwe kama kiingilio kwa kumuona Diamond maana wahusika walisema bila kadi hautaingia ukumbini wakati ni uzushi mtupu maana hakuwepo Diamond wala Ruby na matokeo yake ikala kwao kuna watu wana miaka kibao hapa hata Jay Z hawajamuona LIVE sasa huyu Diamond hata ukimsubiria kwenye foleni unaweza kumuona bila shida...Diamond njoo uwape ULAJI hawa JUNK PROMOTERS(wanajijua) waliojitosa CCM ili wale kiulaini

Anonymous said...

mnajiunga na CCM kwa kipi kizuri ilichofanya kwa wananchi huko nyumbani? Hali duni ya uchumi, rushwa, ufisadi na wizi wa mabilioni yalioficha na vigogo wa serikali ya CCM.mmekinbia nchini kwenu kuja Marekani kutokana na sela mbovu za CCM. Mnajifanya mnakipenda chama kwa mazuri yapi? manadanganywa na vinywaji na vyakula na mnakubali kuuza utu wenu wa kusimamia yaliyo mema kwa taifa lenu,,, Hii ni aibu hasa kwa nyie mliokaa nje

Anonymous said...

Mdau umenena. Kweli ni aibu kubwa sana, tena sana. I repeat...shame on you all who joined CCM bila kufikiria mlikotoka. Mimi sio mwanachama wa chama chochote lakini people we need to think, think, think. This is very sad indeed!!! Tukumbuke, duniani tunapita tu. Haya ni makao yetu ya muda. Sasa nyie mliojiunga kwa malengo ya kuchota ili watanzania nyumbani kule waendelee kuwa na hali duni za mahospitali, mashuleni, ulinzi na usalama wa raia, shauri zenu. Hamtafika popote endapo hamtasaidia ndugu zetu nyumbani. Wakina sie tunasema, yetu macho! Tuwe waangalifu na tusifuate mkumbo jamani. I am just saying!

Anonymous said...

hivi naomba kuuliza nini maan ya kuwa nachama ughaibuni manake sielewi je wataruhusiwa kupiga kura kule tanzania au?manake mi naona mashabiki mandazi tuuuu wabongo tubadilike na mkae mkijua ni kitu gani kimewapeleka huko ughaibuni na kama bado unaipenda ccm kwanini uliondoka tanzania ukaenda ughaibuni kaa jiulize maswali mengi then ushadadie,mnaacha kutafuta SSN mnabakia kusherehekea vyama havitawasaidia chochote kuna mwenzenu kadanganywa na mkubwa mmoja serikalini arudi atatafutiwa kazi kurudi huko olaaa yuko kijijini kwao analima mihogo,na hapo kuna wabongo ambao ni raia wa marekani hata na hao wananjifanya ni ccm thats crazy acheni ujinga na jmn tubadilike.

Anonymous said...

Napenda kutoa machache,Watu wanashindwa kuelewa kwanini Watanzania wa USA wamebadilika. kwanza wamekosa muelekeo pia hawana cha kufanya hata ukiangalia watu wengi waliokuwepo ni watu waotegemea miujiza siku moja Mungu anione. Kama kweli watu wanamammbo ya maendeleo ya kufanya hawawezi kukanyaga hapo maana hakuna cha kujivunia wala cha kusheherekea. MUNGU HIOKOE TANZANIA NA WATU WAKE.