ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 7, 2012

WANDISHI MBEYA KUTOANDIKA HABARI ZA 88


Nadhani hoja hapa sio ya Mkuu wa mkoa wala posho! Hoja hapa ni namna gani mwandishi wa habari anavyoweza kuandika analysis nzuri kuhusu maonyesho hayo ya nane nane hata pasipo kutumia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya!

Ubunifu wa mwandishi wa habari na umahiri wake wa kujua issues katika maonyesho hayo hayo ya  nane kutamfanya awe maarufu na mahiri mara mbili! Hii maana yake nini? Hata hiyo posho itamfuata mwandishi ambaye ameandika habari zihusuzo KILIMO na WIMBO wa siku nyingi kuhusu MAONYESHO HAYO YA KILIMO.



Hapa tunamtaka mwandishi aje na ISSUES kwa mfano, ni kwanini KILIMO kimeendelea kumnyonya mkulima badala ya kumkomboa? Ni kwanini mkulima hana soko la uhakika la bidhaa zake? Ni kwanini mkulima amekuwa anawekewa vikwazo vya kuuza mazao yake pale anapopata soko nje ya nchi? Serikali inamsaidiaje katika hili? Cha ajabu Serikali kupitia kwa viongozi wake ( MA-DC na MA-RC) imekuwa mahiri katika kukwamisha juhudi za mkulima kujikomboa katika KILIMO.

Mimi kwa mfano ningefurahi kama waandishi wa habari wa mkoa wa MBEYA, wangenda mbali zaidi na kuacha kulaumu kwa KUTOPEWA HOTUBA YA MKUU WA MKOA ABBAS KANDORO na kuchimbua issues kutokana na tafiti walizozifanya kuhusu kuandika habari za kilimo! Maana kawaida mwandishi lazima uwe mtafiti kwa kila unachofanya ili uwe OBJECTIVITY katika STORY na FEATURE ZAKO UNAZOANDIKA, VINGINEVYO MTAENDELEA KUTOA LAWAMA TU!

Kuna issues mfano za pembejeo, mfumo wa stakabadhi ghalani na Vocha za pembejeo, nilitegemea KWA MFANO, wakati huu wa maadhimisho ya nane nane mkoani Mbeya, mwandishi akaandika makala kwa kuwaibua wakulima waliofanikiwa katika kilimo na ambao hawakufanikiwa na ni kwanini aki-reflect mambo niliyoyaorodhesha hapo juu.

Kwa mfano maadhimisho ya miaka hii ya nane nane huwezi kuyalinganisha na yale ya miaka ya 70, ambapo walikuwepo wakulima wa mfano, nakumbuka mwaka 1984 nikiwa bado shule ya Msingi niliwahi kuona BOGA KUBWA katika moja ya maadhimisho hayo ya nane nane, VIAZI na MIHOGO ya kutisha lakini leo hii hivyo vyote havipo.

TULIKUWA TUNAONA MIFUGO( KONDOO, MBUZI NA NG'OMBE YA KUTISHA) Leo hii mazao hayo yote ya kilimo na mifugo hayapo! Mwandishi angeenda sasa upande wa pili wa shilingi kuwaeleza wananchi na wakulima wa mbeya na Serikali kwa ujumla kwanini tija katika mazao ya KILIMO na Mifugo imeshuka na sio kama ile iliyokuwa ikionyeshwa miaka ya 70 na 80.

Aeleze kuna tatizo gani akioanisha na mipango ya zimamoto ya Serikali kuhusu kilimo na sio kulalamikia kutopewa posho na hotuba ya mkuu wa mkoa! Hebu watu wa MEDIA tuhame huko,

Nina imani kabisa mwandishi ambaye angeandika hata makala moja kuhusu hayo niliyoyaeleza hapo juu atakuwa LULU na atafuatwa na GARI na posho mlima kama ambavyo wasemavyo wahenga.

Haya kazi kwenu waandishi wa Mbeya, hebu andikeni hata makala moja kuhusu mipango ya zimamoto kuhusu namna Serikali inavyomuendeleza mkulima kuhusu kilimo. Andikeni halafu muone impact ya stories na makala mtakazoandika,ila tu ziwe ni habari zilizoshiba na kufanyiwa utafiti wa kina, lakini kulalamika kuwa hamjapewa hotuba ya RC MBEYA mnajimaliza wenyewe, kwani naamini hata hiyo hotuba ya KANDORO ina mambo ya kuremba na kuikinga Serikali dhidi ya madudu ambayo imekuwa ikifanya kuhusu kilimo. 

Hapo MUPO WAANDISHI WA MBEYA? 
THIS IS A CHALLENGE TO ALL OF YOU!!

No comments: