Kijana Christopher Kule na babake Dasiel Raul |
Kama kuna rais ambaye watu wengi Uganda wangetaka kukutana naye ni rais wa Marekani Barack Obama.
Kijana Christopher Kule, mwenye umri wa miaka
kumi na ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi wilayani Kasese, nchini
Uganda, hajaachwa nyuma katika ndoto hiyo
Bila shaka wengi watasema yuko hatua
nyingi mbele ya wale walio na ndoto ya kumuona Obama. Hii ni baada ya
Kule kupokea majibu ya barua aliyomwandikia Rais Barack Obama kutoka kwa
Obama mwenyewe.
Kijana huyo anaamini kuwa baada ya kuandikiana barua na Rais Obama, kuna matumaini kwamba siku moja atakutana naye.
Yote haya yanatokana na zoezi la kuandika barua
ambalo Kule na wanafunzi wenzake walikuwa wanafanya darasani, baada ya
kuagizwa na mwalimu wamwandikie barua mtu yeyote wakiomba msaada kwa
jamii yao.
Barua ya Kule bila shaka ilimtia hamasa mwalimu wake wa kigeni kutoka Marekani ambaye alikuwa anafunza shuleni humo kwa muda.
Mwalimu huyo alisema kuwa nyanyake ni rafiki wa
mmoja wa wasaidizi katika ikulu ya rais na kuahidi kuhakikisha kuwa
ujumbe huo utamfikia rais Obama na bila shaka ahadi ikatimizwa , kwani
barua ilimfikia rais Obama.
Kule alisema kuwa katika barua yake, alimwomba Obama kusaidia Uganda kuangamiza uasi na kuhamasisha amani.
Katika majibu yake kwa Kule, rais Obama alisema
kuwa Marekani imejitolea kuangazia maswala kadhaa muhimu kote duniani
kama haki za binadamu kwa sababu Marekani inapinga vikali ghasia na
ukandamizaji dhidi ya watu wote. Pia alimtumia kijana huyo picha yake
aliyokuwa ametia saini.
Rais Obama alipata muda wa kumjibu kijana Kule.
Je marais wa Afrika wana muda wa kuzungumza na wananchi wao na kutoa
mfano wa Obama kwa Afrika? Nini maoni yako? Sema nasi katika ukurasa
wetu wa Facebook bbcswahili.
No comments:
Post a Comment