ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 20, 2012

HUDUMA YA ELIMU MTANDAO KUPITIA MAKTBA YAWAFIKIA WANAFUNZI WA CHANGO'MBE MSINGI


Meneja Mradi wa shirika lisilo la kiserikali kutoka Ujerumani ( EIFL) Monica ELBERT, akiwaangalia baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Chang’ombe Mazoezi wilaya ya Temeke jijini Dar- es- Salaam, wakati wakifanya mafunzo ya pamoja jinsi ya kutumia teknolojia ya upashanaji wa habari na mawasiilano kupitia mtandao. 
Mradi huo wa mafunzo ujulikanao (Public Library Innovation Programme- PIP- ) Kwa kupitia mradi huo wanafunzi wataweza kupata taarifa mbalimbali kirahisi kwaajili ya masomo yao na taarifa mbalimbali za kila siku, Meneja wa mradi huo amefurafahishwa sana baada ya kuhojiana na wanafunzi hao na kumueleza kwamba ni ukombozi kwao kwani baada ya kumaliza mafunzo, elimu itakuwa imewasaidia sana kuwarahisishia masuala mbalimbali ya masomo pamoja kupata taarifa mbalimbali
Baaadhi ya wanafunzi wakifanya mazoezi.

Baaadhi ya wanafunzi wakifanya mazoezi. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO, na Sufiani Mafoto.

No comments: