Lipumba Ataka Shekhe Ponda Aachiwe Mara Moja
Mwenyekiti
wa CUF Prof Ibrahim Lipumba ameitaka serikali kumuachilia kwa dhamana
Sheikh Ponda Issa Ponda kwani amewekwa ndani kinyume na utaratibu.
Prof Lipumba amedai kusema kwamba Sheikh Ponda alihusika na uchomaji wa
makanisa ni uongo na kitendo cha kumkamata ndicho kilichochochea vurugu
zilizofanyika wiki iliyopita.Amesema ili kurejesha amani na kunusuru
nchi kuingia katika mfarakano ni lazima kwanza kiongozi huyo wa waislam
aachiliwe huru.
Source:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment