ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 10, 2026

MUHIMBILI YAWEKA HISTORIA, YAFANIKISHA UPASUAJI WA KWANZA WA KUTENGANISHA MAPACHA WALIOUNGANA AINA YA PARASITIC CONJOINED TWINS

 

 

Madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo, Agosti 10, 2026, wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza wa kutenganisha mapacha walioungana aina ya parasitic conjoined twins, ambapo mmoja wa mapacha hakukua kikamilifu na alikuwa akimtegemea mwenzake kwa ukuaji na uhai.

Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Dkt. Victor Ngotta, Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa MNH, amesema mafanikio hayo yanaonyesha uwezo wa hospitali kushughulikia kesi ngumu na adimu zinazohitaji utaalamu wa hali ya juu, na ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha huduma za upasuaji wa kibingwa nchini.

Dkt. Ngotta amesema upasuaji huo ulihitaji maandalizi ya kina na ushirikiano wa wataalamu kutoka fani mbalimbali kutokana na hali ya kipekee ya mtoto huyo, ambaye alikuwa na pacha aliyekuwa na mikono, miguu na sehemu ya kiuno pekee huku akimtegemea mwili wa mwenzake kwa ukuaji na uhai.

Mafanikio ya upasuaji huo yanaendelea kuimarisha nafasi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kama kituo kinachoongoza nchini katika utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi. Mtoto anaendelea vizuri na yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.








No comments: