![]() |
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, ametembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo katika viwanja vya tamasha hilo, Kizimkazi, Zanzibar.
Mhe. Mwinyi amefanya ziara hiyo mapema leo, Agosti 12, 2026, mara baada ya kufungua rasmi tamasha hilo linalofanyika kwa siku tatu, kuanzia Agosti 12 hadi 14, 2026.
Katika ziara hiyo, Rais Mwinyi alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na huduma na fursa zinazotokana na sekta ya maliasili na utalii.
Tamasha hilo linahusisha uzinduzi wa miradi ya maendeleo, maonyesho ya biashara, michezo, pamoja na shughuli za kutangaza utamaduni, utalii na fursa za uwekezaji.
Tamasha la Kizimkazi mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo “Kizimkazi Kumenoga.”




No comments:
Post a Comment