
Asalaam Alaykum!
Saa 4 asubuhi nilifika Central Police kusimamia mahojiano yake na Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO daada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10 kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni hawakumfanyia lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi.
Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:-
1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
i. kwanini waliandamana
ii. nani aliandaa mabango
iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda kumng’oa Mufti na Ndalichako
iv. nani aliandaa maandamano
Sheikh alikiri kuhamasisha maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani aliyaandika hayo mabango. Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.
2. Kuvamia kiwanja cha chang’ombe
Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.
3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu
4. Vurugu mbagala.
Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi.
DHAMANA.
Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo. NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WASIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA
Maasalamu!
By Brother Juma Nassoro – Wakili
3 comments:
Huyu mnayemuita sheikh ana mamlaka gani na nchi hii? Huyu anayehamasisha watu wavunje makanisa na kuiba ndiyo sheikh huyo? waislaam mnapotezwa na watu wasio na hekima, Kwa nini serikali inamvumilia hadi leo? Hii serikali yetu ni dhaifu ndiyo maana anasumbua sumbua, ila nadhani kuna siku isiyo na jina atakuja kujuta.
Haya ni maoni binafsi hayana nia mbaya na dini/imani/mtazamo wa/ya msomaji yeyote.
Ndugu Watanzania, Shehe Ponda na baadhi ya wenzake wamegundua kuwa serikali iliyopo madarakani ni dhaifu na inaweza kuyumbishwa.....watakavyo. Udhaifu huo umeambukiza mpaka vyombo vingine vya dola navyo kuwa goi goi katika kutekeleza majukumu yake.
Ukiangalia vyema utaona kuwa, Shehe Ponda anataka kuhalalisha uhalifu wake binafsi kuwa suala la kidini. Kuhamasisha mandamano bila taratibu au vibali husika, kuvamia maeneo wakati taratibu zipo, kuvunja makanisa au hata kuvamia miskiti ambayo ina uongozi ambao wao hawautaki, kuadhibu watuhumiwa, kushinikiza mamlaka za serikali kutekeleza matakwa binafsi, kutoa matamshi yasiyo kuwa na chembe ya ukweli, kugonganisha waumini wa dini tofauti,kutunishiana misuli na serikali nk
Inabidi ifike wakati....uvunjaji wa sheria ushughulikiwe kisheria kwa wale wote wanaohusika bila kujali dini, itikadi au ufuasi wa chama au kabila lake.
Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa jamii ya Watanzania hivi sasa inakabiliwa na matatizo mengi ambayo sasa yanaibua chuki za kitabaka, kidini, kikabila, kikanda, kichama, kiitikadi nk Wajinga wachache wanataka kuitumia fursa hiyo kuipoteza kabisa amani kiduchu tuliyo nayo na PONDA na kundi lake ni mingoni mwa hao. Angalia vyema aina ya watu wanaojitokeza kushabikia uvunjifu wa amani pale "shehe" huyo anapo hamasisha uvunjifu wa amani [Takbir]...ni watu "waliochoka" kimaisha [kwa sababu mbalimbali] ambao si kwamba ni watu wa dini moja bali hao ndio hujitokeza kuitikia wito wa kiongozi wa dini. Watu wa aina hiyo [wachovu] pia wapo katika dini nyinginezo. Ikumbukwe kuwa mtu aliyekata tamaa ya maisha huamii chochote anachoambiwa na hasa na viongozi wa dini.
Watanzania, ni vyema tuka kaa chini kuamua mwelekeo wa taifa letu ambalo linakabiliwa na matishio ya aina mbalimbali mingine yanaweza kuepukika. Dini ni njia tu ya kumfikia muumba. Watu wa dini zote ambao wanaonekana kutishia umoja wetu, mshikamano wetu, udugu wetu na ustawi wa taifa letu wanatakiwa kushughulikiwa kwa taratibu sahihi. Ushabiki wa kidini na kichama utatufikisha mahala ambapo wengi wetu hatutaki kwenda.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
mnahaki wadau wenzangu kuandika mliyoyandika lakini hamna haki kabisa kuseam kwaba serikali hii ni dhaifu,japo kuwa najua mtapinga hilo kwamba mnayo haki ya kusema mkionacho bila ya kutafakari kwa kina, je walivyouliwa waislamu the mwembe chai kiling serikali ilikuwa strong juu yao siyo dhaifu, je walivyouliwa zanzibar imekuwaje, ilivyochomwa quran sherikali dhaifu, MNAFANYA HAYA KWA SABABU MTAWALI NI MUISLAMU NA HAPENDI KABISA JAMBO HILI MNATAKA MTAWALA AWE WENU DAIMA NA WAKANISANI msilete hapa za kuleta mmezidi kuwaonena sana waislamu lakin sasa wamesha amka na mpaka kieleweke.
mme mtekha sheik farid mmempeleka bara unadhani hatujui.
eti serikali dhaifu mkitawala nini na kuwaonea watu na kuwakandamiza serikali inakuwa strong mnawazimu .
safarihi mtakiona chenu na mungu anakuubuweni si mliabiwa mkitaka kujua nani kachoma makanisa zanzibar mfanye uchunguzi mbona padri wenu kakimbia waongo wakubwa na wanafik sana nyinyi lakin mungu atakulipeni infact kisha kulipeni because kila mnavyotumia nguvu na mabavu na uonevu wenu mungu anazidi kuwaubua mapadri wenu na waku wenu,duniani kote.
katu abadan uislamu uko juu na utazidi kuwa juu na katu abadan hatowayumbisha tena waislamu kama mlivyo zoea na aliiye na macho habiwi tizama kila mtu anaujua ukiristo jinsi ulivyo ndo maana wazungu wa kweli walio soma na kubobea humuoni kwenda kanisani siku ya jumapili,someni historia yenu ya dini yenu BELIEVE PAUL AU JESUS,
aliye na akili atajua asiye na akili anaye sukumwa na ujinga wake aliyie pata kuzungwa toka zamani mashuleni basi atashikilia ujinga huo huo
daima waislamu wako juu na wataendelea kuwa juu ndo maana mnawafuata wao kwenda arabuni kuwaomba
Post a Comment