Picha Juu na chini imechukuliwa Cherry Hill Rd, Beltsville, Maryland kwenye saa 2:50 asubuhi kwa saa za Eastern Time hali inavyoonekana asubuhi hii ni mvua inayoendelea kunyesha watabiri wa hali ya hewa wamesema maeneo ya DMV yamewekwa kwenye tahadhali ya kupata mafuriko mvua inayotarajiwa ni 8" shule, usafiri wa anga, usafiri wa treni na mabasi umesitishwa hasa kwenye jiji lisilolala ya NYC zikiwemo shughuli za serikali. Majimbo mengine yaliyowekwa katika tahadhali ni New York, New Jersey, North Carolina, Delaware, Connecticut na Massachusetts mameya wa majimbo hayo tayari wameisha waonya wakaazi wa maeneo yao watulie nyumbani Hurricane Sandy inasemakana ndio kubwa katika historia ya Marekani na inaambatana na mvua kubwa, upepo mkali unaoenda mile 80 kwa saa
No comments:
Post a Comment