ANGALIA LIVE NEWS
Wednesday, October 24, 2012
MBINU ZA KUDUMU NA STAA KWENYE UHUSIANO!
UMEWAHI kujiuliza; kwanini mastaa wengi hawadumu na wenzi wao? Nimeamua kuchambua mada hii kwa sababu tunao mastaa wengi kwenye jamii yetu ambao wana uhusiano ama na mastaa wenzao au watu wa kawaida.
Pia, wapo watu ambao wanatarajia kuwa na uhusiano na mastaa, wakati kuna ambao tayari wapo ndani ya penzi na watu maarufu. Pamoja na hayo yote, wengi huwa wanashindwa kudumu kwa muda mrefu na mastaa kwa sababu za hapa na pale.
Katika mada hii ambayo nimeifanyia utafiti wa muda mrefu, itakufanya mpya katika uamuzi wako, ndani ya uhusiano na staa au staa ambaye yupo katika uhusiano na mwenzi asiye staa.
Labda tuwekane sawa kidogo, hapa namzungumzia mtu maarufu katika jamii, maarufu kwa maana ya kujulikana sana. Ustaa wa mtu unaweza kusababishwa na kazi au sanaa. Mathalani, sanaa za maigizo, soka, ndondi, riadha, siasa, urembo, utangazaji, uandishi wa habari, mitindo, utunzi, uchoraji, uchongaji, biashara nk.
Siwezi kutaja moja kwa moja majina ya mastaa, lakini naamini nimeeleweka vyema kuwa nawazungumzia watu wa aina gani. Watu wanaojulikana sana katika jamii kulingana na kazi zao za kila siku.
WASIKIE MASTAA
Wakati naandaa mada hii, nilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya mastaa ambapo walitoa maoni yao. Kwa bahati mbaya sana, wote niliopata kuzungumza nao, walipojua mazungumzo yetu yangeishia kuwa mada gazetini waliomba kuhifadhiwa majina yao.
Hebu wasikilize: “Kiukweli kaka Shaluwa, naweza kusema sisi wanawake wenyewe ndiyo wenye matatizo...asikudanganye mtu, ustaa kazi. Ukishakuwa maarufu, unataka mambo mengi; vipodozi, gari, nguo mpya, kujirusha, simu iwe na full vocha nk.
“Sasa kama unakuwa na boy ambaye anajifanya anakuchunga sana, inakuwa ngumu kudumu na sisi tulivyo jeuri, akikuacha asubuhi, jioni kiwanja unakutana na mwingine.”
Huyu ni staa wa muziki wa dansi nchini kama alivyozungumza nami jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Kiukweli huwa tunaacha sana mademu, lakini siyo suala la umalaya hapo brother Shaluwa. Kuna mambo mawili makubwa; kwanza, mwanamke anakuwa anapenda ustaa wako na siyo penzi la dhati, pili anakubana na kukupangia sana ratiba...niseme kwamba, wivu unazidi!
“Unajua unapokuwa msanii, unakuwa na mambo mengi, shoo kibao kila week-end, safari za mikoani nazo hazina idadi, club ndio usiseme, sasa kwa hali hiyo, lazima uwe na mwanamke smart kwa kila kitu.
“Tuongee ukweli, hakuna mtu anayekubali kuwa na mpenzi tapeli, sisi hatuna matatizo, lakini kama umefuata jina langu au pesa, nitakushtukia soon na hapo ndipo nitakapompiga kibuti na maisha yanaendelea,” ndivyo mmoja wa kinara katika Bongo Fleva anavyosema.
Hebu sikia kauli ya msanii huyu wa filamu: “Wanawake wanapenda umaarufu wetu, kwahiyo ukiwa naye siku mbili, ukimshtukia unamtema, hapo ndipo penye tatizo bro. Mimi sihitaji mtu anayependa jina langu, nahitaji penzi la dhati.”
TATIZO NI NINI?
Kikubwa ni katika KUELEWA na kutofautisha mapenzi na ustaa. Kama umempenda, umpende kwa mapenzi ya dhati, achana na ustaa wake, lakini lazima umjue mwenzi wako na uende naye jinsi anavyotaka.
Mapenzi ya kitapeli au kufuata mali na umaarufu hayana nafasi kabisa katika maisha ya sasa, yote yanawezekana lakini kwa kukubali kujifunza na kubadilika kulingana na mwenzi wako alivyo.
UPO KWENYE UHUSIANO NA STAA?
Kama nilivyotangulia kusema awali, sina maana kwamba mastaa wote hawawezi kuishi na wenzi wao bila kuwepo kwa migogoro, ni baadhi yao! Pamoja na kuwa na migogoro hiyo ambayo mwisho wake mara nyingi imekuwa ni kuachana, hakumaanishi kwamba, mastaa hawafai kuwa na wapenzi.
Hapa nataka kuzungumza na wale ambao tayari wapo katika uhusiano na mastaa na wale ambao wanatarajia kuwa na wenzi wenye majina makubwa kwenye jamii. Hebu pitia vipengele vifuatavyo;
Usiwe na wivu sana!
Ni kweli kwamba, kati ya alama za mapenzi ya dhati ni pamoja na wivu, lakini unapokuwa na uhusiano na mwenzi staa, lazima upunguze wivu. Hii haina maana kwamba, umuache awe kicheche, awe na mapatna wengi, hapana!
Mara nyingi mastaa huwa wanaiga mambo ya Kizungu, mathalani husalimiana kwa kukumbatiana, kuandikiana sms kwa maneno ya mapenzi kama dear, sweetie, mpenzi n.k, ukikutana na mazingira kama hayo, kuwa mpole, lakini fanya uchunguzi wako taratibu bila ya yeye kujua. Penye ukweli, uongo hujitenga.
Nafasi yangu kwa leo imeishia hapa, wiki ijayo tutaendelea.
www.globalpublishers.info
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment