Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema shirika la viwango la Zanzibar (ZBS) bado halijaanza kazi ambapo watendaji wake wamekuwa wakipata mafunzo mbali mbali huko Tanzania Bara kupitia kwa shirika la viwango TBS.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Thuwaiba Edington Kisasi wakati akijibu swali lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Chake chake (CUF) Omar Ali Shehe aliyetaka kujuwa kwa nini hadi sasa shirika la viwango bado halijaanza kazi zake tangu sheria ya kuanzishwa kwake kupitishwa na baraza la wawakilishi.
Kisasi alisema sheria ya kuanzishwa kwa shirika hilo imepitishwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi na kutiwa saini na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi lakini kwa sasa baadhi ya mambo muhimu ikiwemo wataalamu bado hawajapatikana.
“Shirika la viwango la taifa limepitishwa na baraza la wawakilishi na rais kutia saini mswada wake ambapo tayari mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo ameteuliwa.....lakini tatizo kubwa ni kwamba bado hatuna watendaji na wataalamu wa kufanya kazi za shirika kwa sasa”alisema.
Kisasi amesema serikali imepitisha sheria ya kuanzishwa kwa shirika la viwango zanziba katika kusimamia viwango vya ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa matumizi.
Alisema katika kutekeleza sheria hiyo raisi wa zanziba na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mhe: dkk ali mohammed shein amemteuwa mkurugenzi wa shirika hilo na hatua za awali zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kumpatia mkurugenzi huyo mafunzo ya namna ya utekelezaji na majukumu ya shirika hilo huko tanzaniabata.
Alisema hatua nyengine zinazochukuliwa ni kutayarisha kanuni na muundo wa shirika hilo na mpango mzima wa utekelezaji wa shughuli za shika la viwango zanzibar.
Kisasi alisema kwa upande mwengine serikali imetenga bajeti na eneo maalum kwa ajili ya kuanzia shughuli za shirika hilo huko maruhubi katika eneo lililokuwa kiwanda cha sigara na tayari michoro ya ujenzi wa eneo hilo zinaendelea kufanyika.
amefahamisha kuwa kwa sasa imapotokezea inapotokezea kupatikana kwa bidhaa zikiwemo vifaa vya umeme vyenye kutiliwa mashaka juu ya ubora wake bidhaa hizo hupelekwa katika shirika la viwango la tanzanibara (TBS) kwa ajili ya kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo kabla ya kutumika.
Alisema watendaji wa shirika hilo akiwemo mkurugenzi mkuu wapo ziarani Tanzania Bara kwa ajili ya kujifunza shunguli mbali mbali za kazi za shirika hilo,ambalo miongoni mwa majukumu yake makubwa kusimamia ubora wa viwango kwa bidhaa zinazoingizwa nchini.
Alisema kwa sasa wizara ya biashara inaendelea na kazi za kuchunguza na kudhibiti bidhaa zinazoingizwa nchini ikiwemo kupitia bandarini kwa ajili ya kujuwa ubora wake kabla ya kutumiwa na wananchi.
Kisasi alisema jengo la ofisi ya shirika la viwango lipo Maruhubi ambapo kwa mujibu wa bajeti ya wizara ya biashara viwanda na masoko kwa mwaka wa fedha shirika hilo litaingiziwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake.
No comments:
Post a Comment