ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 22, 2012

SHUKURANI ZA DHATI

Tunapenda kutoa shukurani zetu kwa Watanzania DMV na wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine na hatimae kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu Clarrise Maya Niyonkuru.

Kusema ukweli tumefarijika sana na sisi sote wanafamilia, jamaa na marafiki wa karibu wa Maya tunajivunia kuwa miongoni wa Jumuiya ya DMV tunafahamu mpendwa wetu hakua mwanachama wa Jumuiya lakini wanajumuiya wakiongozwa na Viongozi wao walisimama kidete na kuhakikisha Mtanzania mwenzao anazikwa kama Mtanzania mwingine kusema ukweli tumeguswa sana na tunasema asante na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie saba mara sabini.

Mwisho tunapenda kuvishukuru vyombo vyetu vya kuhabarisha hapa DMV kwani mchango wao mkubwa umewezesha na hatimae kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu Baraka za mwenyezi Mungu ziwe pamoja na nyie, daima awatie nguvu, awaongoze na kuwapa ujasiri kwani tunatambua kazi yetu si rahisi pia niyakujitolea na jumuiya nzima inawategemea lakini mlitafuta muda wa kuitaarifu jumuiya ya DMV, Marekani na Dunia kuhusu msiba huu na maendeleao yake tunasema asante sana kwa kazi yenu nzuri na moyo wenu wa kujitolea ni mfano wa kuigwa.

No comments: