SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inawasaka walimu bingwa wa sayansi waliostaafu na kuwashawishi kuchukua mikataba ya miaka miwili ili kusaidia sekta ya elimu katika somo la sayansi.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna amesema hayo jana katika kikao cha baraza la wawkailishi kinachoendelea ambapo alisema wizara ya elimu inahitaji walimu bingwa kwa ajili ya kusaidia somo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limekosa walimu wazuri.
Shamhuna alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura (CCM), Hamza Hassan Juma aliyetaka kujuwa kwa nini walimu waliostaafu hawachukuliwi na kuajiriwa kwa masharti ya mkataba.
Shamuhuna alisema wizara haina vikwazo vya kuajiri walimu wenye uwezo wa kusomesha masomo ya sayansi waliostaafu kazi kama watakuwa tayari kufanya kazi hiyo kwani imekuwa ikiwatafutalakini wengi wao umri wao ni mkubwa na wamekuwa wakikataa kwa kuwa muda wao wa kutumikia serikali imepita na wanahitaji kupumzika.
“Mheshimiwa Naibu Spika sisi msimamo wa wizara ya elimu kwa walimu waliostaafu kazi kurudi kazini na kufanya kazi kwa mkataba upo wazi.....walimu wanaotaka kurudi kazini kusomesha kwa mkataba wapo huru kufanya hivyo na wizara inatoa mkataba wa miaka miwili lakini tatizo kubwa ni kuwa tunapowapata huwa ama umri wao unakuwa ni mkubwa au huwa wanakataa kwa kuwa wanataka kupumzika” alisema Shamuhuna.
Aliwatokea mfano wajumbe hao kwamba wizarailiwahi kumfuata mwalimu mmoja ambaye ni bingwa mkubwa wa masomo ya sayansi aliyestaafu katika shule ya Haille Sellasie ambapo aliombwa kurudi kazini baada ya kustaafu na kuahidiwa kupewa mshahara mnono na kutunzwa lakini alikataa kwa sababu ya kuwa hawezi kurudi tena kazini kwa kuwa anataka kupumzika.

Alisema baadhi ya walimu waliostaafu kazi hawapo tayari kurudi kazini kufanya kazi licha ya kuahidiwa kupewa mkataba monono,ambapo wengi wanataka kubaki kama wastaafu na kupumzika baada ya utumishi serikalini.
Shamuhuna alisema kwa sasa serikali inafanya juhudi mbali mbali ikiwemo kuomba walimu wa masomo ya sayansi kutoka nje ya nchi ili kuziba pengo la upungufu wa walimu wa masomo hayo ambapo katika mwaka 2012/2013, wizarainakusudia kuajiri walimu 1,000 wa masomo mbali mbali ikiwemo sayansi kwa ajili ya skuli za msingi na sekondari.
“Maombi ya uajiri wa walimu hao yameshawasilishwa tume ya utumishi serikalini kwa ajili ya kufnayiwa kazi na wizara ipo tayari kuwaajiri walimu hao mara tu taratibu za tume ya utumishi za uajiri zitakapokamilika” alisema Shamhuna.
Alisema bado serikali imekudia kuajiri walimu kutoka Nigeria, India na Misri ambao ni mabingwa kwa masomo ya sayansi lakini alisema wakitoka hapa hapa nchini itakuwa vyema na serikali inaahidi kuwaajiri kwa ajili ya kuendeleza masomo ya sayansi.
No comments:
Post a Comment