ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 23, 2012

Spika Makinda ashiriki Mkutano wa 127 wa IPU, Mjini Quebec, Canada. Akutana na Spika wa Morocco


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina ya Global Fund na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua Nderakindo Kessy kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali na maazimio ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Kwa picha zaidi bofya read more

Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti wa Bunge Ndg. Kileo Nyambele anaye muwakilisha katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashilila akishiliki kikao cha makatibu wa Mabunge yote wanachama wa Mabunge ya Dunia (IPU) katika Mkutano wa 127 wa chama hicho mjini Quebec, Canada. Kulia kwake ni Afisa dawati la IPU kutoka Tanzania Ndg. James Warbarg.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa Tanzania kupiga kura kuingiza agenda mojawapo kati ya agenda 5 za dharura zilizowasilishwa kwa udharura katika mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) ili zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika kupigia kura agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali pamoja na agenda iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa udharura swala la hatma ya Usalama na Misaada wa Kibinadamu Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.

Spika wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Mhe. David Kafulila anayehudhuria Mkutano huo pia.

Mhe. Anne Makinda akitoka katika Mkutano na Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Karim Ghellab kwa lengo la kufanya nae mazungumzo ya faragha kuimarisha uhusiano baina ya mabunge ya Tanzania na Morroco.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati alipokutana na Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab kujadili namna bora ya kuimarisha mahusiano baina ya mabunge ya nchi zao. Tanzania ilipeleka ujumbe wa Wabunge kutoka kamati ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama kutembelea Bunge la Morocco Aprili mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo.


Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini mada kuhusu “Multilateralism and the role of parliament in parliamentary diplomacy” wakati wa mkutano huo Mjini Quebec, Canada.

No comments: