ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 4, 2012


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

October 4, 2012

Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) linapenda kuwatangazia mapromota, mameneja pamoja na wadau wote wa ngumi katika ukanda huu kuwa kuanzia leo tarehe 4 Octoba 2012 ubingwa wote wa (ECAPBA) utaishi kwa kipindi cha miezi minne tu!

Aidha, kuna taratibu mpya za kuandaa ubingwa wa ECAPBA na wale walio mabingwa mpaka sasa mwisho wa ubingwa wao ni mwezi wa 12. Baada ya hapo watatakiwa watetee ubingwa na taratibu mpya za ECAPBA.

1. Kuanzia sasa mabondia wote watakaogombea ubingwa wa ECAPBA ni lazima wawe wameshapigana mapambano
    yasiyopungua 8. kati ya hayo mawili ya raundi 4, mawili ya raundi 6, mawili ya raundi 8 na mawili ya raundi 10.

2. Kabla ya mpambano wenyewe ni lazima majina na rekodi za mabondia watakaocheza zikubaliwe na ECAPBA

3. Waamuzi wote watakaosimamia mapambano haya ni lazima wapitishwe na ECAPBC

4. ECAPBA haitaruhusu pambano kutangazwa kabla ya kupata kibali chake.

Haya yote yanafanyika ili kulinda viwango na maisha ya mabondia pamoja na wadau wanaoshiriki katika kuuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati.

Imetolewa na;

Onesmo Alfred McBride Ngowi

Rais,

Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)

Dar-ES-Salaam, Tanzania

No comments: