.jpg)
Mgomo ya Yanga kuvaa jezi zenye nembo nyekundu za Vodacom hatimaye umepatiwa ufumbuzi baada ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya huduma za simu, Rene Meza, kusema "hakuna tatizo, kilichopo ni kukosa mawasiliano tu."
Mwaka jana Vodacom iliafiki kuwatengenezea Yanga jezi nembo nyeusi baada ya mabingwa hao wa soka Afrika Mashariki na Kati kuweka wazi msimamo wao kwamba hawawezi kuvaa nembo nyekundu, ambayo ni rangi ya mahasimu wao, Simba.
Akizungumza kuhusiana na suala hilo, Meza alisema kuwa hakuna tatizo lolote katika suala hilo na kwamba watakaa kuongea na kulimaliza.
Mkurugenzi huyo alisema kinachofanya kuwapo na malumbano kati ya Yanga, Shirikisho la Soka Nchini (TFF) na kampuni yao ni kukosekana kwa mawasiliano rasmi ya kumaliza tatizo hilo.
Kuhusu suala la African Lyon kuvaa jezi ambazo kifuani zina nembo ya udhamini wa kampuni pinzani kibiashara ya Zantel, alisema klabu hiyo inapaswa iangalie thamani na uwekezaji uliofanywa na Vodacom kwa ligi nzima badala ya kuangalia upande wake tu.
Alisema kwamba Vodacom imewekeza fedha nyingi kwenye ligi hiyo tofauti na udhamini mdogo ambao kampuni ya huduma za simu ya Zantel imeingia mkataba na timu hiyo.
Kuhusu ulinganisho unaotolewa kwamba klabu ya Liverpool huvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wao binafsi benki ya Standard Chartered licha ya ligi kuu ya England kudhaminiwa na benki ya Barclays, Meza alisema suala hilo ni la kimkataba na hakufafanua zaidi.
Yanga na African Lyon ndiyo klabu pekee ambazo zimecheza mechi zao sita bila ya kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini huyo wa ligi na TFF haijatoa adhabu yoyote mpaka sasa, licha ya rais wake Leodegar Tenga, kudai kwamba ni lazima klabu zivae nembo hiyo na itakayokiuka itaadhibiwa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment