ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 17, 2012

WAJUMBE WA CCM WAPATA AJALI MKOANI MWANZA LEO


Wanausalama barabarabani wakipima ajali hiyo iliyosababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni dereva wa basi lenye namba za usajili T 853 BRB lililokuwa na wajumbe wa CCM kutoka wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo.
BASI lililobeba wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutoka wilaya ya Kwimba limepata ajali na kuanguka eneo la Buhongwa wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza majira ya saa 3:30 - 4:00 asubuhi leo.
Basi lenye namba za usajili T 853 BRB lililokuwa na wajumbe wa CCM likiwa katikati ya barabara mara baada ya kupata ajali.
Imeelezwa kuwa dereva wa chombo hicho cha usafiri amefariki dunia papo hapo na wajumbe wengine saba kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi lilikuwa katika harakati za kulikwepa lori aina ya Fusso ambalo lilikuwa likigeuza kujiweka sawa kuingia barabarani ndipo basi hilo lilipopoteza uelekeo na kulibamiza Fusso na kupinduka.
Wajumbe hao kutoka wilaya ya Kwimba, walikuwa wakiingia jijini Mwanza kwenye uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mwanza unaofanyika leo uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la tukio.
Picha/Habari: GSENGO BLOG

No comments: