ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 26, 2012

WAKAZI WA ISANGA MBEYA WAGOMA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDI WAAMUA KWENDA KUFANYA USAFI MAKABURI YA ISANGA

Wakiongea na Mbeya yetu wakazi hao wa isanga wamesema leo hawasherehekei sikukuu ya idi badala yake leo sherehe yao ni kufanya usafi katika makaburi ya isanga na zoezi hili litaendelea kila jumaosi na siku za mapumziko mpaka makaburi hayo yawe safi kabisa
Hakika wazee wengi na vijana wamejitokeza katika kufanya usafi katika makaburi haya ya isanga
Mzee mbio akiwahi kufanya usafi kweli leo wamegoma kusherehekea Idi

Bibi nae hakucheza mbali na eneo la tukio hataki mchezo yupo kukwatua visiki vidogodogo hapo makaburini
Bibi sasa amechoka anasaidiwa jembe
Watangazaji wa Bomba FM Gabriel na Kamanga matukio nao waliungana na wakazi hao wa isanga katika kufanya usafi wa makaburi hayo ya isanga 
Joseph mwaisango wa mbeya yetu hakucheza mbali natukio hilo nae akifanya usafi kuwakilisha Tone Multimedia company Limited

Mbeya Yetu Blog

1 comment:

Anonymous said...

pongezi kubwa kwa waislamu wa Mbeya hapo naona makaburi ya kristo na islamu yote yanasafishwa kwa mujibu wa eid alhaji,wale wahuni wanaojiita waislamu wa siasa kali waone ushirikiano wa watanzania tangu enzi na enzi hao ni waislamu halisi tunaowafahamu wanasafisha makaburi bila kujali ya wakristo au waislamu huu ndio udini tunaoujua wa kupendana sio wao wahuni na sera zao za kupigana mapanga Shehe Ponda wa kundi lako mlaaniwe, mshindwe na mlegee azma yenu mungu aichome moto itokomee kama majivu