Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao
walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba
hili
walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba
hili
NA JOSHUA MWAKABUNGU
Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara liyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha
kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi
watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na
mwekezaji huyo.
kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi
watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na
mwekezaji huyo.
Kamnda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani
1 comment:
mkifanyiwa nyinyi oooh mnaatangaza kote na kulaani pamoja na mapadri wenu mbona kuran ilivyochomwa mbona walivyo pigwa mabomu zanzibar na mwembe chai etc mbona hajawaonea huruma.
sasa mnaonyesha hizi picha ili kuthibitisha kwamba tutalipa kisasi na kumtuma kikwete aende oman ili huku nyuma muwauwe waislamu na dini yao lakini wameshindwa wazungu wenu itakuwa nyinyi watu wa maporini msio na chembe na huruma wala ustaarabu.
mungu atatulipia kwa maonevu yenu
Post a Comment