Balozi
wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, akizungumza na
waandishi wa habari jana kuhusiana na mikakati yake ya kufanya
mazungumza na wafanya biashara mbali mbali wa hapa nchini.
Viongozi wa kinywaji cha Hennesy pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Juu na chini Waandishi wakiwa makini kufuatilia.
Na Mwandishi wetu
Auriol aliwasili jijini juzi na kufanya mazungumza na wenyeji wake kabla ya kuelezea nia ya safari yake ambayo lengo kubwa ni kutanua soko la kinywaji hicho maarufu duniani kwa Watanzania nan chi za Afrika Mashariki.
Alisema kuwa pamoja na kukutana na wafanyabiashara, pia atakutana na watu wa sekta tofauti, miongoni mwao ni wanamuziki na wanamitindo. Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku tano. Alifafanua kuwa ujio wake ni mara ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ameona kuna mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara na hasa katika soko la vinywaji vikali.
Alisema kuwa kinywaji cha Hennessy kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja kwa Watanzania kuanza kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya bora. Ikiwa na zaidi ya historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa kinywaji (Cognac) bora zaidi duniani.
Pia Auriol atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi ya wanawake watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya kinywaji cha Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji hicho lengo likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji hicho wakiwa majumbani mwao.
No comments:
Post a Comment