Waziri wa mambo ya nje
wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields, Mh. David
Miliband akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya
Utalii Tanzania TTB, Bw. Geofrey Meena (kushoto) mara baada ya kumalizika
kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa.
David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya Suderland.
Mkurugenzi
wa Masoko wa
Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields,
Mh. David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa
Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya timu
hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya Jumamosi nchini
Uingereza. Bodi ya Utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa
Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea Ligi Kuu ya
Uingereza (Premier League) ukiwemo Stadium of Light wa Sunderland FC.
Katika
picha katikati ni Edmund Hazal, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech
Services
inayoratibu matangazo hayo. Bw. David Miliband pia ni Mwenyekti wa
Klabu
ya Sunderland.
Mkurugenzi
wa Masoko wa
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi, akiwa katika picha ya
pamoja
na wachezaji wa zamani na maofisa wa timu ya Sunderland FC baada ya
kukabidhiwa zawadi ya saa. Kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na
golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson, Mkurugenzi wa
Biashara, na Kevin Ball nahodha wa zamani wa timu hiyo.
Ujumbe wa Bodi ya Utalii
na maofisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja nje ya uwanja
huo. Kutoka kulia ni Manase kutoka Ngorongoro, Mukhtar kutoka
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Masoko TTB Devotha Mdachi,
Geofrey Meena Meneja Masoko TTB na Edmund Hazal, Mkurugenzi wa kampuni ya
Lantech Services inayoratibu matangazo hayo katika viwanja vya Ligi Kuu
Uingereza.




No comments:
Post a Comment