ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 10, 2012

BUNDI BADO ANAIMBA NDANI YA CLUB YA SIMBA LAKINI BUNDI HUYO HUYO ULAYA ANAFUGWA

Team ya TOTO AFRICA ya Mwanza wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga Simba kwa bao 1, hapa wanaonekana wenye furaha baada ya kumbeba kocha wao juu na kuzunguka nae uwanjani hasa upande waliokaa wapenzi wa Yanga. Toto Africa inasemakana ni ndugu wa Yanga na wanavyocheza na Simba basi hucheza kwa nguvu zote. Hizo ndio Yanga na Simba, ukiona kumoja sherehe basi subiri zamu yako na kwako kunakuja, ndio haya yanayoendelea upande wa Simba sasa baada ya kuanza ligi kwa shangwe na mahasimu wao Yanga kuanza kwa kusuasua
Haya yote yanatokana na timu kutegemea pesa za mifukoni mwa watu na si kujitegemea kama timu kwa kuwa na vitega uchumi. Kama kuwa na viwanja vyenu ambavyo vitawaingizia mapato au kuwa na miradi mingine ambayo hata siku moja msingeweza kutegemea pesa za wajanja wachache wanaofanya hivyo siku wakiwa kwenye mood mzuri, na siku wakinuna au kutofautiana na mchezaji kipenzi timu, au viongozi basi timu mzima inayumba.
Simba na Yanga acheni kutegemea pesa za watu binafsi na jijengeni kimaendelea na kuachana na mambo ya wazee au wanachama wanaoamua mambo ndani ya club mambo yasiyo kuwa na maendeleo zaidi ya kudidimiza mchezo wa mpira wa miguu katika nchi yetu.

No comments: