Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ispekta Jenerali (IGP) Said Mwema
“Uteuzi huu wa IGP Mwema umezidi kudhihirisha namna Serikali ya CCM inavyozidi kupalilia na kukomaza mizizi ya tabia ya kulindana, si katika ufisadi wa mali za umma tu, bali hata katika roho za watu, hasa raia wa kawaida," alisema Lwakatare.
Tamko la chama hicho limekuja baada ya IGP Mwema kufanya mabadiliko kwenye safu ya makamanda na maofisa mbalimbali bila kumgusa wa Iringa, Michael Kamuhanda ambaye amekuwa akiwekewa shinikizo la kuwajibishwa.
“IGP Mwema anaendelea kupanga na kupangua safu yake bila kuzingatia ukweli kuwa Jeshi hilo analoliongoza, liko katikati ya tuhuma za mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu," alisema Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare.
Alidai: Uteuzi wowote unaofanyika bila kuzingatia ukweli huo, hauwezi kuondoa doa kubwa linaloandama jeshi hilo mbele ya macho ya Watanzania."Lwakatare ambaye alitoa maelezo hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema Chadema ingetarajia mabadiliko ya kulisuka upya jeshi hilo kwa kubadili makamanda na maofiosa wengine.
“Uteuzi huu wa IGP Mwema umezidi kudhihirisha namna Serikali ya CCM inavyozidi kupalilia na kukomaza mizizi ya tabia ya kulindana, si katika ufisadi wa mali za umma tu, bali hata katika roho za watu, hasa raia wa kawaida," alisema Lwakatare.
Alisema kuwa Kamati Kuu ya Chadema pamoja na Barua ya Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe kwenda kwa Rais, kumtaka Rais Kikwete ilimtaka awawajibishe viongozi wa juu wa Wizara ya mambo ya ndani kutokana na mauaji yaliyotokea Arusha, Morogoro na Iringa.
Alitaja baadhi ya matukio hayo kuwa ni Januari 5, mwaka huu ambapo watu watatu waliuwawa mkoani Arusha na mto mmoja aliyeuawa Agosti 27 mkoani Morogoro na Mwanindishi wa Habari mkoani Iringa Septemba, 2
Chanzo: Mwananchi

No comments:
Post a Comment