Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq,
Mkuu wa Mkoa aliamua kutoa ahadi hiyo baada ya kuelezwa na uongozi wa shule kuwa kuna watoto yatima 23 shuleni hapo lakini kati yao ni watoto 17 wanawafadhili wa kuwasomesha.
Awali, Mkuu wa shule hiyo Ndele Mwaselela, alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa shule hiyo inatafuta wafadhili wa kusomesha wanafunzi hao kwani shule haina uwezo wa kuwagharamia kila kitu.
“Nitawasomesha hadi elimu ya juu lakini lazima mhakikishe mnafanya vizuri darasani, sitaki kufadhili watu wanaotaka kumaliza shule tu mimi nataka kusomesha mtu mwenye malengo ya kufika mbali kielimu,” alisema aliongezea yatima ni kama walivyo watoto wengine hivyo wanastahili kupata matunzo na elimu sawa na watoto wenye wazazi na aliona jamii kujitolea kuwasomesha.
Vile vile, Sadiq alisifu shule hiyo kwamba licha kumilikiwa na Kanisa lakini inatoa elimu bila upendeleo wowote kwa wanafunzi waislamu. “Kwa hali ya kawaida shule kama hizi unatarajia ukuta asilimia 90 ya wanafunzi ni wakristu lakini hapa ni kinyume chake kwani waislamu ndio wanaonekana wako wengi kuliko wakristu,” alisema
Mkuu wa Mkoa aliahidi kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu ubora wa shule hiyo na namna inavyotoa elimu bila ubaguzi wa dini ingawa inaendeshwa kwa sadaka za wakristu. “HIli jambo zuri sana lazima nimweleze Rais Kikwete namna mnavyotoa elimu bila ubaguzi, wale wanaotaka kututenga kwa misingi ya ubaguzi wa dini waje wajifunze hapa St Patrick,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment