ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 11, 2012

FUMANIZI AMBAZO HAZITOI ADHABU NI SAHIHI?

Mpenzi msomaji,
Leo tujadili kidogo kuhusu fumanizi ambazo hazitoi adhabu. Je. Ni sahihi au siyo sahihi?.

Wiki iliyopita nilipanda kibajadi na kinadada wawili. Kakini pia alikuwepo kijana mmoja pamoja na dereva wa kibajaji hicho. Wakati tukiwa safarini, katika mazungumzo likajitokeza suala la fumanizi.

Hapo kila mtu akatoa maoni yake. Aliyeanzisha jambo hilo alikuwa dereva wa kibajaji ambaye alieleza kituko alichoshuhudia na hivyo sisi wengine tukachangia katika mjadala ule.

Kaka yule dereva akasema ifuatavyo; “Jamaa alimfumania mke wake ndani kwake. Hakufanya fujo zozote mbali na kumwambia mkewe apike chakula ili wale wote na mgeni (dowezi).
Mama kusikia vile akawa anajivuta vuta. Na mama kweli akapika.

Swali: Yule jamaa aliyefumaniwa kusikia hivyo hakufungua mlango akimbie?

Dereva: Akimbie na wakati ali-mtaim. Baada ya kupika chakula akamwita, “mwenzangu njoo tule akawa anajivunga vunga akamwambia njoo ule. Akala hivyo hivyo kwa shingo upande, akamaliza, akamwambia haya nenda.

Huku akiwa haamini, akaondoka. Kisha mwanaume kisha na mkewe. Mwanaume akawa analazimisha maongezi lakini mwanamke roho haipo kabisa anashangaa mbona siadhibiwi?

Wakalala vizuri, mwanaume kesho yake akaenda kazini, kurudi kwani alimkuta mkewe! Alikuta kashafungasha mwenyewe na kuondoka. Alikuwa na mtoto mmoja akaondoka na mwanae.

Kuona vile mwanaume akaenda kumsaka akamkuta kwa wakwe zake. Akasalimia akasema, ‘nimemfuata mke wangu’. Mwanamke akiulizwa kulikoni hasemi, akiambiwa na mumewe twende nyumbani hataki.

Akaulizwa vipi? Jamaa kuuliza kuna nini akasema nilienda kazini kurudi sikumkuta, nimemtafuta kila mahali ndipo nimemkuta hapa. Sasa hataki kurudi nyumbani, hebu muulizeni kosa langu ni nini?

SWALI: (Mchangiaji mwingine akauliza); jamaa yule hakumkong’ota jamaa wala mkewe pengine kutokana na ukweli kwamba hata yeye ni mfuska ana vidosho huko mitaani.

Wengine hujua fika kuwa wanasaliti wake zao hata wakati mwingine hulala nje na kwa maana hiyo huenda mkewe huwa anamkosa ndio sasabu naye anatafuta mwanaume wa nje.

Dereva: Hata hivyo, yule jamaa inasemekana alikuwa akiambiwa siku nyingi na majirani kwamba wakati anapokuwa hayupo, mkewe huwa anaingiza mwanaume ndani. Ndiyo maana siku hiyo akaweka mtego na kuwafuma laivu nyumbani.

Yule bwana alijifanya anasafiri kikazi lakini huku nyuma akarudi ghafla na ndipo alipokuta kiroja kile. Na ni majirani walitoa taarifa kwamba kwa wakati huo mkewe alikuwa na mwanaume ndani kalala na ndipo alipowafuma.

Kule kwa wakwe ikabidi bibie aeleze ukweli kwamba mwenzangu alinifumania na mimi katu sirudi. Hajanipa adhabu yoyote, yule mtu gani. Unajua mtu afadhali akupige ujue yameisha lakini hakuulizi wala hakuadhibu, ina maana hakupendi.

Bora akupige kwani kitendo kile ni kosa. Hata kama ingekuwa ni mwanaume kafumaniwa na mkewe, halafu hamuulizi, je, ni sawa hiyo? Lazima roho ikuume. Ila kusema ukweli kitendo cha kuleta mshikaji wa nje nyumbani ni kosa kubwa.

SWALI: Mwanaume yule anapaswa aulizwe hivi ni kweli anamhitaji mke yule au anataka arudi kisha akamkong’ote? Au anaweza kukurudisha nyumbani lakini akakufanyia visa kwa kukuletea kimwana nyumban kisha akakwambia utulie kimya kama yeye alivyotulia bila kutoa adhabu.

Dada mmoja ndani ya bajaji ile akawa na mfano mwingine akasema: “Yupo baba mmoja alimfumania mkewe hivyo hivyo huko Dodoma. Hakufanya lolote, lakini alichofanya mume ni kumletea mkewe changudoa nyumbani. Changudoa huyo akalipwa hela ya kutosha.

Mama akaambiwa kaa hapo wakaingia ndani baba na changudoa wakatia stori za dunia ili tu mama aumie roho. Kisha jamaa akaingia kazini kimapenzi na yule changudoa huku mkewe anatizama sinema ya bure.

Mama akitaka kulala anapigwa na kuambiwa lazima aangalie kila kitu kinachofanyika, mwishowe alizimia. Mama yule inasemekana aliachana na yule mzee moja kwa moja.

Wanaume ukimkosea wanaweka rohoni lakini sisi wanawake tunaongea sana lakini mtu akiongea sana anatoa kitu rohoni kulikoni yule mtu anayehifadhi vitu rohoni. Mwanamke hana sehemu ya kuhifadhia lakini mwanaume anaweka rohoni.

Mwanaume anakuwa na vinyongo. Kuna kutosahau lakini kuna kuumia ndio maana watu wanakufa haraka”.

Mpenzi msomaji, hayo ndiyo niliyoweza kunasa wakati wa mazungumzo yale kabla sijateremka kwenye kibajaji kile. Je msomaji wangu, fumanizi ambazo hazitoi adhabu ni sahihi? Toa maoni kuhusiana na mazungumzo hayo. Karibu uchangie na ukiwa tayari, kuwa huru kutuma ujumbe mfupi kupitia simu ya ofisi namba 774268581(usipige), au barua pepe; fwingia@gmail.com

Kumbuka kama hutapenda jina au simu yako itajwe gazetini tamka hivyo na hilo litaheshimiwa.

Wasalaam.
CHANZO: NIPASHE

No comments: