Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China leo.
Katika Mradi huo wa Teknohama itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari na Vyuoni kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma mbele maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUAWEI kutoka China Bw. Bruce Zhang akizungumza katika hafla hiyo kwamba Mpango huu unaoitwa "Huawei ICT Star" itasaidia katika shule za Primary na Sekondari katika kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania.
Alisema katika Program hii itasaidia kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na Teknolojia ili kutoa mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na Teknolojia.
Balozi wa China nchini Tanzania Mh. LU YOUQING akitoa maelezo yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa Teknohama katika shule na vyuo nchini Tanzania.
Balozi alisema mpango huu ni mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China katika nyanja mbalimbali za biashara uchumi na Kijamii.
Aliongeza kwamba Serikali ya China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015.
Meza Kuu.
Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa China wakizindua rasmi mpango wa "HUAWEI ICT STAR" nchini Tanzania.
kwa picha zaidi bofya read more
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Bw. Bruce Zhang wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.
Profesa Mbarawa akimkabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.
Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi.
No comments:
Post a Comment