Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi, katika Uwanja wa Soko Kuu mjini Mtwara, leo akiwa katika ziara ya siku moja mkoani humo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwahutubia viongozi wa CCM ngazi mbalimbali mkoani Mtwara, alipokutana nao kwenye ukumbi wa Makonde mkoani humo, akiwa katika ziara ya siku moja kutembelea mashina na matawi ya CCM na kufanya mikutano ya hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Mjumbe wa Shina namba mbili, katika kijiji cha Mkunwa Mtwara vijijini leo katika ziara ya siku moja kutembelea mashina na matawi ya CCM na kufanya mikutano ya hadhara mkoani humo.
(Picha na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment