Kipre Balou anamtoka Othman Tamim (Picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog)
Kocha wa Yanga Ernest 'Ernie' Brandts amekisifu kikoisi chatimu ya Azam FC watakachokutana nacho kesho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Bara kuwa kina wachezaji wenye uwezo mkubwa.
Akizungumza kwenye uwanja wa Azam Complex mara baada ya mchezo kati ya Azam na Coastal Union juzi, Brandts alisema licha ya Yanga kuwa kwenye kasi kwa sasa, watakuwa na kazi ngumu mbele ya timu hiyo.
"Nawafahamu Azam tangu kwenye mashindano ya Kombe la Kagame, na leo nimepata nafasi ya kuwaona tena," alisema Brandts na kueleza zaidi kuwa "ni timu nzuri na inayocheza soka la kisasa kwa sababu wachezaji wake wana stamina na wanacheza soka la nguvu."Kwa kweli tutakuwa na kazi ngumu kwenye mchezo wetu wa Jumapili (kesho)."
Aidha, alisema kuwa atatumia mapungufu aliyoyaona kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Coastal Union kuhakikisha kikosi chake kinapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kesho.
Alisema katika kikosi hicho cha Azam, ambayo juzi iliifunga Coastal 4-1, anamuhofia mshambuliaji John Bocco.Aliema mchezaji huyo anajua kufanya kazi yake na kwamba kwake itakuwa furaha kama atakosekana kwenye mchezo huo.
Hata hivyo, habari ambazo Nipashe imezipata na kuthibitishwa na msemaji wa Azam, Jaffar Iddi, Bocco atakuwepo kikosini kesho baada ya kupona majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kichapo cha magoli 3-1 dhidi ya Simba wiki iliyopita.
"Bocco anaendelea vizuri na hakuna shaka Jumapili (kesho) atakuwepo uwanjani kutegemea na kocha atakavyoamua... ila yuko vizuri baada ya kupona majeraha yake," alisema Iddi.
Kocha huyo wa Yanga alisema wachezaji wake kwa sasa wapo katika hali nzuri kimwili na kiakili; hasa baada ya kuibuka na ushindi mfululizo kwenye ligi kuu wakifuta machungu ya kuanza vibaya katika michezo minne ya mwanzoni mwa msimu.
Azam itaikaribisha Yanga kesho kwenye Uwanja Taifa, ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa timu hizo tangu mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati hao waifunge timu hiyo ya wauza vyakula 2-0 kwenye fainali ya Kombe la Kagame Julai.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment