Si ugonjwa unaosababishwa na kirusi, hapana. Ni gonjwa la maneno litakaloshambulia ubongo wake. Kila mara kabla ya kuingia kwenye mchezo atakuwa na maswali ya kujiuliza. “Sijui leo nitashindwa tena?” “Nikishindwa itakuwaje?” “Atanitukana tena?” “Hivi mimi ni mgonjwa?”
Mwisho wa maswali hayo atahitimisha kauli kwa kusema: “Inawezekana mimi ni mgonjwa kweli ndiyo maana nashindwa kazi.” Amini kuwa kauli hiyo ndiyo ugonjwa hatari ambao utashambulia hisia zake na kuusababisha mwili ushindwe kufanya kazi sawasawa.
Ukitaka kuendelea kufurahia mapenzi ni vizuri umpe moyo mwenzi wako pale inapoonekana ameshindwa kutekeleza kazi ya faragha inavyotakiwa. Kaa naye vizuri na umueleze kwa lugha laini kwamba baadaye au siku inayofuata mtafanya tena kikamilifu na hakutakuwa na kushindwa.
Ikibidi msifie, mwambie kuwa yupo kamili kwa sababu kila siku mnapoingia kazini huwa unatosheka. Mueleze kuwa siku hiyo unasumbuliwa na uchovu au hujisikii vizuri. Maneno hayo utayaona madogo lakini yatamjenga ipasavyo. Yatamrejeshea ari na afya, kwa hiyo siku nyingine hatakuogopa.
Mapenzi ni matamu lakini siyo rahisi. Hii imesababisha watu wengi kushindwa kushirikiana vema na wenzi wao. Jambo dogo la kumuelewesha mwenzake linakuwa tatizo mpaka uhusiano unageuka shubiri. Wawili walioitana majina matamu na yenye kupendeza, wanageuka maadui.
Wanatangaziana sifa mbaya. “Yule muoneni hivyo hivyo kwa nje, hajiwezi kabisa kitandani.” Ni maneno ambayo si mageni. Yanasababishwa na watu kutotambua thamani ya mapenzi, ugumu uliopo ili iwe rahisi kwao kupata alama A kwenye uhusiano wao. Mapenzi ni magumu lakini ni rahisi sana.
Kanuni ni moja tu, kuwa mwelewa. Unaona mwenzi wako anashindwa kukufikisha unapopataka, wewe una jukumu la kumwelewesha. Mfahamishe maeneo ambayo anatakiwa ayafanyie kazi ili ufurahie tendo. Amini kuwa ukifanya hivyo, itakuwa rahisi kwako. Mapenzi ni matamu kama utayajua na kuyaweza.
Kuna maswali ya kujiuliza kuhusu mapenzi. Hayo ndiyo yatakuwezesha kutambua kama unatosha kuendelea na mwenzi wako au kinyume chake. Yatakusaidia kufurahia maisha yako ya kimapenzi.
Mapenzi ni matamu lakini siyo rahisi. Mada hiyo niliyoiandika kwenye gazeti hili kwenye matoleo yaliyopita ndiyo imeleta muendelezo huu. Hii ni sehemu ya pili na lengo lake ni kuushinda ugumu uliopo na kuyaweza mapenzi kwa asilimia 100.
Jambo la muhimu ni kwamba usije ukaingia kwenye uhusiano ukidhani kila kitu ni chepesi. Unatakiwa kujipanga, halafu uwe mdadisi kisha upite njia inayostahili.
Ugumu mkubwa ambao upo kwenye mapenzi ni pale mtu anapotaka aoneshwe upendo kulingana na jinsi anavyopenda. Inapotokea anabaini tofauti kati ya anavyopenda na anavyopendwa inakuwa shida kubwa. Hataki kupenda zaidi, eti ataonekana wa bei nafuu.
Kila mtu anataka apendwe zaidi. Kwa nini wewe usiwe wa kwanza kujitoa kumpenda mwenzi wako kuliko yeye anavyokupenda? Ni mtihani mdogo lakini unawashinda wengi na kusababisha mvutano.
Uzoefu unaonesha kuwa watu wengi hawana imani na wenzi wao. Dosari ndogo inaweza kuwafanya wajenge imani kuwa wenzi wao hawawapendi. Kila mmoja analalamika kivyake. “Hanipendi kama mimi ninavyompenda.” Ugumu wa mapenzi huanzia hapo.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment