MH. Balozi Tuvako Manongi na MH. Naibu mwakilishi wakiwa kwenye kikao na viongozi wa Tanzania NY Community, Katika kikao hicho cha utambulisho kwa viongozi hao kwa balozi na kumfahamisha rasmi jukumu la kuwa mlezi wa viongozi na jumuiya. Mh. Balozi alikubari wazifa huo kwa moyo mweupe na kuhaidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi hao kwa kadri ya uwezo wake wote akishirikiana na Mh. Naibu mwakilishi Ramadhan Muombwa Mwinyi. Nakatika kikao hicho Mh. Balozi Manongi alikabizi kwa mwenyekiti wa jumuiya bwana Hajji Khamis mwongozo kuhusu utaratibu wa watanzania wanaoishi ughaibuni kushiriki kutoa maoni yao kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.
Hapa Mh. Naibu Mwakilishi Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akifafanua jambo mbele ya viongozi wa jumuiya katika kikao hicho, Mh. Muombwa alipata pia fursa ya kukutana na viongozi wa Tanzania NY Community kwa mala ya kwanza. Viongozi wa jumuiya walimkaribisha NY na atakuwa bega kwa bega na viongozi hao kadri ya uwezo wake kama ilivyo kwa Mh. Balozi Manongi kuakikisha kila kitu kilichozungumzwa hapa kina enda sawa kama kilivyo pangwa kwa manufaha ya community.
Kikao kikiendelea kuna mweka azina wa community bwana Temba, katibu wa community bwana Shaban Mseba, mwenyekiti wa community bwana Hajji Khamis na dada Lydia Jengo-Waluye kama mjumbe mwenye mtazamo wa kimaendeleo.
MH. Balozi Manongo akimkabizi mwenyekiti wa jumuiya bwana Hajji Khamis mwongozo kuhusu utaratibu wa watanzania wanaoishi ughaibuni kushiriki kutoa maoni yao kuhusu upatikanaji wa katiba mpya
Kutoka kushoto ni mweka azina wa community na CEO wa Temba Engineering, akifuatiwa na Mh. Balozi Manongi akikabizi mwongozo huo kwa bwana Hajji Mwenyekiti wa Jumuiya na mwisho ni Mh. Naibu mwakilishi balozi Muombwa wakishuudia makabiziano hayo yaliyo fanyika katika office za Ubalozi New York City.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho kumalizika officini hapo, kama kumbukumbu
Katibu wa jumuiya bwana Mseba akipata Ukodak na Mh. Naibu Mwakilishi balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi baada ya kikao
CEO Temba Engineering na mweka azina wa community akipata Ukodaki na Mh. Naibu Mwakilishi balozi Ramadhan Muombwa baada ya kikao.
Mwenyekiti wa jumuiya bwana Hajji Khamis akipata Ukodak wa kumbukumbu na Mh.
Bwana Shaban katibu wa community akipata Ukodak na Mh. Balozi Manongi |
Ny Ebra nae akipata Ukodak na waheshimiwa kwa heshima na tahazima |
3 comments:
nataka kujua jamani anaye ijua CV YA BWANA HAJJ KHAMID NI NINI NA IPI BECAUSE NAONA NDO ANAYETUWAKILISHA WATANZANIA HAPA NY SO TUJULISHENI NA MTUWEKE WAZI SIYO MAMBO YA KUJUANA NA TU NA KUPACHIKANA KATIKA UONGOZI kiholela holela kwa mantiki ya ushikaji wa kujuana
huyu NY Ebra yani hata hajui sehemu za heshma kuvaa kinidhamu kila leo yeye kujibambika tu kujifanya mzungu mweusi
Hawa watu walichaguliwa na nani au wamejipachika wenyewe tuu, hiki chama ni bomu wanampotezea balozi mda wake wa kufanya kazi muhimu.
Kwanza kabisa, Maafa ya Zanzibar yalipotokea tulichanga pesa za kuwasaidia ndugu zetu huko Zenji, Chama cha NY hawajasema mpaka leo walikusanya kiasi gani na nani alikabithiwa kuzifikisha kwa ndugu zetu.
Pili, sherehe na kumuaga mama Migiro tulizotwa dola 30 kuingia, tulitoa ili kuwenda kumuaga kiongozi wetu lakini mpaka leo hakuna aliyesema ni dola ngapi zilikusanywa na zimewekwa kwenye mfuko gani ili ziendelee kukisaidia chama.
Tatu, Mheshimiwa waziri mkuu na mke wake, Mheshimiwa waziri wa mambo ya nchi za nje na viongzi wengine walifanya harambee miaka miwili iliyopita na kuchanga zaidi ya dola 15,000 kukisaidia chama cha NY lakni mpaka leo hakuna lolote lililosemwa kuhusiana na pesa hizo.
Sass mnataka tena tutoe dola 25 kuja kuwakaribisha hawa waheshimiwa, sasa swali ni kwamba je, hiyo TRANSPARENCY iko wapi??????
Je, hawa viongozi wa NY ni kweli wanataka kuongoza au wanataka kukamilisha mambo yao binafsi???
Jamani wakati umefika wa kuwajibika kwa viongozi hawa wa sasa.
Kama wanataka chama kisonge mbele lazima pawepo na UWAZI kutokana kuwa chama chenyewe bado ni kichanga na pia kinahitaji watu ambao watakuwa viongozi ambao wana nia ya kukiendeleza na wala sio kukifanya kuwa mradi wao binafsi.
Huko nyuma tulikuwa tunaishi bila chama lakini tulikuwa tunakutana na kuchoma nyama zetu bila tatizo.
Katiba mpya iandikwe, tuchague viongozi wapya na tuanze mambo mapya la sivyo hatufiki popote.
Post a Comment