Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatahadharisha wananchi kutoshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ili kuepusha uwezekano wa kutiwa mbaroni kwa sababu hayana kibali.
Maandamano hayo yamepangwa kufanyika leo ( na kesho kushinikiza Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda, na wenzake wanaokabiliwa na mashtaka mbalimbali kupewa dhamana.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akizungumza na NIPASHE jana, alisema Jeshi la Polisi halitakuwa na uvumilivu wa aina yeyote kwa vitendo vya fujo na vurugu vitakavyosababishwa na watu watakaodhubutu kuandamana na badala yake hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Kova alisema kwenda mahakamani kwa maandamano ni sawa na kuingilia uhuru wa mahakama, hivyo Jeshi la Polisi litahakikisha linaimarisha ulinzi katika Mahakama ya Kisutu na kuweka utaratibu wa kiwango cha watu watakaoruhusiwa kuingia mahakamani hapo na watakaokiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema wazazi wasiruhusu watoto wao kwenda mahakamani ili wasije wakakumbana na kamatakamata kwa sababu sheria inayohusu watoto inakataza watoto kutojihusisha katika shughuli yeyote inayovuruga amani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, alisema hakuna sababu yeyote kwa waumini wa dini ya Kiislamu kufanya maandamano hayo kwani kufanya hivyo ni kuchochea vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani.
Aidha, Sadiki alisema madai ya Waislamu yote yana fanyiwa kazi kuhusu Sheikh Ponda ni suala la mahakama kwa hiyo haitakiwi kuingilia masuala ya mahakama ambayo inafanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Hatua ya serikali na Jeshi la Polisi kutoa tahadhari hiyo inafuatia kuwepo kwa vipeperushi vilivyosambazwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania vinavyowataka Waislamu kushiriki maandamano ya kesho.
Vipeperushi hivyo vina ujumbe unaoeleza kuwa “watukufu Waislamu mnaarifiwa maandamano makubwa ya amani yatakayofanyika siku ya Ijumaa mara baada ya swala ya Ijumaa kuelekea ofis ya Waziri Mkuu kwa Dar es Salaam, mikoani yataelekea kwa Wakuu wa Mikoa na kwa Zanzibar yataelekea Ofisi ya Makamu wa Rais”.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment