ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 7, 2012

Serikali yasema ‘kuchimba dawa’ porini ni aibu

Wasafiri wakijisaidia porini, jambo linalokataliwa na serikali kwani ni tendo la aibu
"Kitendo cha cha abiria kujisaidia njiani wakati wa safari ‘kuchimba dawa’, ni kitendo cha aibu na kinadhalilisha utu wa mwanadamu"

WIZARA ya Uchukuzi imetangaza kuwa kitendo cha cha abiria kujisaidia wawapo njiani katika safari zao ‘kuchimba dawa’, ni kitendo cha aibu na kinadhalilisha utu wa mwanadamu.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tzeba wakati akijibu swali la Joyce Mukya (Viti Maalum- Chadema).
Dk, Tzeba alisema kuwa kitendo hicho pia kinatoa picha mbaya kwa wageni wanaotembelea Tanzania huku ikiwa ni hatari kwa ajili ya majambazi pamoja na wanyama wakali.

Alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), ilishatoa tamko la kuzuia abiri kuchimba dawa wawapo safarini kwa kutumia sheria namba 9 ya mwaka 2011 vifungu vya 5 (f) na 6 (4).

Katika swali la msingi Mukya alitaka kujua ni sheria gani iliyotumika kutoa tamko la kuzuia uchimbaji dawa na kuhoji serikali imeweka miundombinu gani mbadala ya kuwezesha huduma hiyo muhimu kuwa safi.

Pia alitaka kujua iwapo serikali haioni kuwa inawanyima haki za msingi baadhi ya abiria ambao kutokana na maradhi ya kisukari, homa za matumbo na wajawazito hutakiwa kupata huduma hiyo mara kwa mara.

Naibu Waziri alisema kuwa imefanya utafiti katika njia mbalimbali za barabarani na kubaini kuwepo kwa maeneo mazuri na rasmi yaliyojengwa na Halmashauri za Miji, Mikoa, Wilaya pamoja na watu binafsi kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.

Alisema ukwa katika mazingira ya utoaji wa huduma hiyo, serikali imezingatia makundi yote muhimu kwa ajili ya kuwawekea miundombinu ya kutosha kwa ajili ya huduma hiyo pindi wawapo safarini.

Kuhusu mabasi kuwekewa vyoo, Naibu Waziri alisema ni mpango na utaratibu wa watengenezaji wa mabasi hayo kwani mabasi mengi hadi sasa hayana huduma hiyo ambayo inaonekana kuwa ni muhimu sana

Chanzo:Mwananchi

4 comments:

Anonymous said...

Jengeni Rest areas! Toeni Tenda watu waje wajenge rest areas kwa kujusaidia, sasa wafanyeje??? na wamebanwa?

Anonymous said...

waweke vyoo kwenye mabasi? hiyo inabidi kuwepo kwa system nzuri ya ku-empty hivyo vyoo otherwise utashangaa wanavi-empty huko huko mwituni. tanzania kwa kupenda kufanya mambo kama vile nchi zilizoendelea! wanakaa bungeni badala ya ku-discuss mambo ya muhimu kama vile tatizo la maji, umeme na barabara, wenyewe na magari mbona huwa wanachimba dawa vile vile au na magari yao yawekewe vyoo basi

Anonymous said...

Waache tu wawe kama India watu milioni 600 hawana vyoo wao ni kuchimba dawa 24/7.

Anonymous said...

aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhhhh!!! KWI..KWI...KWI....CHEKA MIMI.....AAAAAHHHHH!!!!!