ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 15, 2012

YULE MTOTO ALIYEUNGUZWA MKONO NA KULISHWA KINYESI NA MAMA YAKE MDOGO AKATWA MKONO

HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO KABLA YA KUKATWA MKONO JANA
Bahati Rukangara huyu ndiye aliyemchoma mtoto Janeth Mkono wake wa kushoto
MTOTO ANETH AKIWA ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUMKATA MKONO WAKE WA KUSHOTO JANA
KWA UJUMLA MTOTO ANETH SASA ANAENDELEA VIZURI NA ANAKULA CHAKULA VIZURI PIA TAARIFA TULIZOPATA MUDA SI MREFU MAMA YAKE MZAZI YUPO NJIANI KUJA MBEYA TOKA KAGERA
ANETH AKUTAYARISHIWA CHAKULA NA MAMA YAKE MDOGO SLIVIA ANAEMUHUDUMIA HOSPITALINI HAPO.Habari naVenance Matinya, 

HALI ya Mtoto Aneth Johanes (4) aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kufuatia kuchomwa moto mkono wake wa kushoto na anayedaiwa kuwa ni Shangazi yake inaendelea vizuri licha ya kufanyiwa upasuaji uliolazimu kukatwa kwa mkono huo.

Kwa mujibu wa mama mdogo wa mgonjwa anayemhudumia hospitalini hapo Silvia Salvatory alithibitisha kuendelea vizuri kwa motto huyo ambapo alisema ilimlazimu kufanyiwa upasuaji kutokana na mkono huo kukosa mawasiliano na kuonekana kuvunjika.
Alisema taarifa za awali zinaonesha shangazi yake huyo Bahati Rukangara alianza kumtesa mtoto huyo muda mrefu mara baada ya kumchukua kutoka kwa wazazi wake wanaoishi Bukoba Mkoani Kagera.

Aliongeza kuwa tangu amchukue kwa wazazi wake Februari Mwaka huu amewahi kumjeruhi mkono wake wa Kulia hadi kuuvunja ambapo hadi sasa mtoto huyo alikuwa akitegemea mkono wa kushoto ambao umekatwa.

Tukio hilo la kisikitisha lilitokea juzi majira ya saa nne asubuhi baada ya majirani kusikia yowe la mtoto huyo akiomba msaada kutokana na mateso na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhabu hiyo kutoka kwa Shangazi yake

Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Thomas Isidori alisema hali iliyopelekea kukatwa kwa mkono wa mtoto huyo ni siri kati yake na daktari aliyemhudumia na kwamba sheria ya uuguzi inakataza kutoa taarifa ambazo ni siri.

Isidori alipoulizwa sababu za mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji mapema mno hadi kusababisha ulemavu alisema ni suala la kitaalamu ambalo hata yeye hawezi kulijibu na ni sheria ambayo inawataka madaktari kutunza siri za wagonjwa.

Hata hivyo muuguzi huyo alizuia kabisa waandishi wa habari kupiga picha za motto huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo uliosababisha kukatwa mkono kwa mgonjwa huyo.

Baadhi ya wananchi waliofika Hospitalini hapo kumjulia hali mtoto Aneth aliyelazwa Wodi namba Nane ambao hawakutaka kutaja majina yao walilaani kitendo cha madaktari kukimbilia kukata mkono mgonjwa badala ya kujaribu njia zingine za kunusuru hali hiyo.

KUNA UTARATIBU MAALUM AMBAO UNAANDALIWA HIVI SASA JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO ANETH KWA MSAADA WOWOTE AMBAO WADAU WETU WATUKUFU MTAKUA TAYARI KUTOA/KUJITOLEA, ENDELEA KUDURUSU UKURASA HUU KWA UPDATE ZA MARA KWA MARA ZA HALI YA MTOTO ANETH

2 comments:

Anonymous said...

WHY,KWA NINI ATAKUWA AMEFANYA NINI? HUYU MAMA LAZIMA ANAKICHAA. HIVI NYUMBANI KUNA HUMAN RIGHTS KWELI.POLE,POLE SANA ANETH UTAPONA MDOGO WANGU.

Anonymous said...

Hili tukio limeniumiza moyo wangu kwa kiwango cha juu sana. Kwa kweli kuna binadamu wana mioyo ya kinyama. Hiiimevuka mpaka.

KP