Ssentongo akimtoka beki wa Sudan Kusini
Beki wa Sudan Kusini akimpitia kwanja kiungo wa Uganda, Joseph Ochaya
Mashabiki wa Uganda kwa raha zao
Beki wa Kenya, Abdallah Juma akimsukumia kitu cha mbavu Nahodha wa Ethiopia Fikru Teffera Lemessa katika mchezo wa mwisho wa Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda. Kenya ilishinda 3-1, mabao ya Ramadhan Mohamed Salim, Clifton Miheso na David Ochieng, wakati la Ethiopia lilifungwa na Gatech Panom Yietch. Kenya imeungana na Uganda kutinga Robo Fainali na sasa Ethiopia wataiombea Sudan Kusini ifungwe na Uganda katika mchezo unaofuata, ili wao wajaribu hata kuwania kupita kama mmoja wa washindi wa tatu bora.
Shabiki maarufu wa Kenya Juma kutoka Nakuru
Kocha wa Tanzania Bara, Mdenmark Kim Poulsen akiwa na shabiki wa kike wa Tanzania wakati wanaangalia mchezo wa Kenya na Ethiopia.
Katibu wa CECAFA, Nocholas Musonye wakati anaangalia mechi ya nchi yake, Kenya na Ethiopia
Ramadhan Mohamed Salim wa Kenya, akimtoka beki wa Ethiopia Mehari Mena Medelcho katika mchezo wa mwisho wa Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda. Kenya ilishinda 3-1, mabao ya Ramadhan Mohamed Salim, Clifton Miheso na David Ochieng, wakati la Ethiopia lilifungwa na Gatech Panom Yietch. Kenya imeungana na Uganda kutinga Robo Fainali na sasa Ethiopia wataiombea Sudan Kusini ifungwe na Uganda katika mchezo unaofuata, ili wao wajaribu hata kuwania kupita kama mmoja wa washindi wa tatu bora.
Anthony Kimani akimtoka Mehari Mena Medelcho
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
UGANDA wamefuzu kwa asilimia 100 hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kushinda mechi zake zote za Kundi A, ikiwemo ya leo waliyoshinda 4-0 dhidi ya Sudan Kusini.
Hakuna mjadala, Sudan Kusini inaondoka katika mashindano haya, bila kuingiza hata pointi moja, wakifungwa mechi zote tatu.
Uganda na Kenya wamefuzu moja kwa moja, wakati Ethiopia walioshika nafasi ya tatu watasubiri hatima yao kufuzu kama mmoja wa washindi wa watatu bora kutoka makundi yote, A, B na C.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Uganda ambao pia ni mabingwa watetezi yalifungwa na Brian Umony mawili katika dakika za 23 na 39, Robert Ssentongo dakika ya 47 na Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 79.
Katika mechi ya kwanza, Kenya ilishinda 3-1 dhidi ya Ethiopia, mabao ya Ramadhan Mohamed Salim, Clifton Miheso na David Ochieng, wakati la Ethiopia lilifungwa na Gatech Panom Yietch.
Michuano hiyo, itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B na C, saa 8:00 mchana, Tanzania Bara watamenyana na Somalia Uwanja wa Lugogo na baadaye saa 10:00, Rwanda itacheza na Eritrea wakati Sudan itaanza na Burundi saa 8:00 mchana Uwanja wa Wankulunkulu na baadaye saa 10:00 jioni Malawi watamenyana na Zanzibar Wankulunkulu.
Kikosi cha Uganda kilikuwa; Ali Kimera, Robert Ssentongo, Joseph Ochaya, Kweyune Said, Henry Kalungi, Isaac isinde, Manco Kaweesa/Joseph Mpande, Geoffrey Kizito, Nico Wakiro Wadada, Brian Umony/Brian Majwega na Hamisi Kiiza.
MSIMAMO KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
Uganda 3 3 0 0 6 0 6 9
Kenya 3 2 0 1 4 2 2 6
Ethiopia 3 1 0 2 2 3 -1 3
Sudan Kusini 3 0 0 3 0 7 -7 0
Habari na picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog
No comments:
Post a Comment