| Filamu Mpya ya Cultural Wars Sasa Yapatikana! Wahi Kujipatia DVD! |
Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars” iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York, New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy”
Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”, Ny Ebra aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka “Chemponda” na Isaac Kibodya aka “Father”. Wote mliosaidia katika kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za dhati kabisa.
Usikose kujipatia nakala yako kwa kuinunua au kuiona kupitia link hapa chini:
24 comments:
Safi Sana Watanzania wa New York kwa Kuweka Historia hii. Tunapenda sana kusika habari za mafanikio na za kujivunia kama hizi za utengenezaji wa Filamu. Kama mtaweza itakuwa vizuri muendelee hivyo hivyo ila kuweza kutuburudisha Watanzania wa ughaibuni. Mimi binafsi nimefurahishwa sana na habari hii.
Big Up sana Director Mhella. Usipunguze kazi. Wewe na timu yako endeleeni kutuburudisha. Na mimi nikitoka hapa naenda online kununua DVD ili nikupe support. Wasanii wanahitaji support yetu. Watz tutoe support yetu kwa Mtanzania na Watanzania wenzetu wanapofanya mambo mazuri kama haya.
Is this real? I can't believe it! Hurraaaay Guys!
Sijawahi kusikia a full-length movie from New York, directed by a Tanzanian! Wow! Congratulations! This is a milestone.
Ndugu Mhella hongera sana ... Tulikuwa wote London na sasa naona umeamua kufanya kweli... Do you remember professor Lynch? He used to say "always aspire for higher heights", You got it brother. You and your team congratulations!
Hivi Ibra nae yupo? Nimekaa mkao wa kula ila nikucheki brother. Kipaji unacho! Mpira mtuachieni DC, ila filamu tunawaachia NY.
Mr. Film Director, I'm in it next time you film another one. I am Judy we met in Philly two weeks ago. Just let me know.
Diamond the Platinumz, nasikia huko Marekani. Ongea na hawa vijana utoe nao moja ya movie babu K.
Sasa ni New York Stars Versus Bongo Stars! Nani zaidi?
Haya ya mpira jamani yame kujaje tenaaa. Hunimafano wa kuigwa kazi nzuri mtunzi na team yako tuta kuunga mkono ta mtanzania yoyote mwenye fikra kama hizi tuko tayari kuwaunga mkono.Kazi nzuri
Baada baada ya kuiona hii trailer nanunua DVD yangu kesho. Hii imekaa vizuri sana!
Vijana mmethubutu na mmeweza. Sasa songeni mbele hakuna kurudi Nyuma.
Napenda kushirikiana kwenu na wasanii wa filamu wa kimarekani Kwani wao wamebobea katika gani hii. Mkiendelea nao mnaweza kufika mbali. Hakikisheni hamuwapotezi.
This is great! Watoto wetu wasirudie makosa tuliyofanya sisi.
Mdau hapo juu hujakosea. Madingi mengine noma kichizi, yakisikia una mchumba wa kimarekani, kasheshe linaanza. Halafu Ukipata huyo Mbongo wanaomtaka akisha kuchoka baada ya miaka miwili anakuolea mke mdogo au Nyumba ndogo. Sasa si bora uoe au uolewe na Yule akupendae?
Mimi niliolewa na dume la Kimarekani na familia ya upande wangu wakaja juu. Ikabidi tuachane. Lakini bado nampenda yule bwana na kila siku moyo wangu unaumia kwa nini niliachana nae.Ni jamaa mzuri tu na pochi analo. Ila ndio hivyo wandugu wakaja juu. Eti akienda kijijini huyu atakunywa maji kwenye kibuyu, na atakula ugali wa mhogo kwa mlenda? Mbona Marekani na hata Bongo tunachagua vyakula tule nini tunachokitaka, sasa huyu akijichagulia ndio iwe nongwa? Yaani mambo mengine yananiumiza roho, natamani wakati urudi nyuma nirudiane na mpenzi wangu niliyeachana nae. Niliolewa na mbongo na kaniletea nyumba ndogo ndani ya nyumba na sasa nasikia kapata dogo dogo mwingine TZ, maana safari zake za TZ haziishi, akisingizia anafanya biashara. Hii filamu inazungumzia masuala ya kweli. Inabidi tuanze kubadirika ili haya yasije yakawakuta watoto wetu.Tuwape uhuru wa kupenda ili maisha yao yawe bora.
Mkuu hawa wabongo huwa hawanunui vitu vya wabongo wenzao. Utakuja niambia.
lini itawekwa greatlakesmix? lol...i am just joking. anything inahusiana na Ibra hata million nitatoa...good job my people
na iam not joking nataka mimi nione kwenye the greatlakes mix sina uwezo wakuinunua so tuambiyeni au hamtoiweka mnataka kutengeneza fedhaaaaa.
Nishapata copy yangu. Mhella umefanya kazi nzuri. NY Ibra bosi wa Brooklyn nimependa acting yako. Nyote mmefanya kazi nzuri. Ijayo itangazeni mapema tuweze kushiriki.
Baada ya kuwafahamu waigizaji wa Movie hii kutokana na juhudi mliyoifanya ya kuwatangaza kwenye vijimambo nami nimeafiki na naikubali movie hii kuwa ni ya kiwango cha juu.
Just got a copy for my son.Good acting,and great job Ny actors,Ibra you rock in this movie,this is your calling keep it up.
Jeez, si bora mngeandika nakala ya kwenye gazeti kuliko kutengeneza filamu ambayo ni kama maigizo ya primary. Hao actors yaani ni sifuri kwenye uigizaji kabisa. Nakubaliana na ujumbe ila wafikishaji ujumbe hii si fani yao kabisaaa!! Ukweli nimesema niueni.
Watanzania hivi kwa nini wana roho mbaya sana duh .hebu nunueni DVD hizo muache WIVU na uzushi .support wenzio .
Post a Comment