Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioachishwa kazi.
ASKARI wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliopiga picha ya mahaba wakibusiana huku wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi na picha yao ikasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii wamefukuzwa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe amethibitisha leo kwa waandishi wa habari mkoani humo kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.Kamanda Mwaibambe amezungumza na ITV na kusema askari hao walitenda kosa hilo la fedhea kwa kupiga picha kinyume na maadili ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na kwamba PC Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya mkononi na kuituma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi.
1 comment:
Hakuna budi kutima vyeo vya maaskari hao. Isije ikawa kwamba askari wa kike alishurutishwa na Wakuu wake ama aliogopa kukubali tendon hilo. Wanasheria mnasemaje
Post a Comment