Tabia ya msichana mmoja kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja hasa kwa maeneo ya mjini imekuwa ni kama fasheni. Unaweza kusema upo peke yako kwa huyo uliyenaye lakini kumbe mko wawili.
Hii ni kwa sababu wengi wao wanafanya usaliti kwa umakini mkubwa sana bila ya wanaume kushtukia huku tamaa ya fedha na vitu vya thamani vikiwa ndiyo chanzo.
Matokeo yake unakuta msichana mmoja anakuwa na mwanaume wa kumlipia kodi ya nyumba, wa kumfanyia ‘shopping’ na wa kumlisha.
Wenye tabia hiyo wengi wao ni wale wasichana wazuri ambao wakikatiza mbele za wanaume ni lazima wapate usumbufu wa hapa na pale. Hawa wanapokosa msimamo wa kusema ‘no’ kwa wanaume wanaowatokea, matokeo yake ndiyo hayo ya kuwapanga foleni wanaume.
Kinachoniuma sasa ni kwamba kuna wanaume ambao wao wanatafuta wanawake wa kuoa na wanapokutana na wasichana hawa, hujikuta wakiwekeza ile mbaya wakidhani wamebahatika kupata wasichana wazuri kumbe wameingia ‘vyoo vya kike’.
Ukitaka kujua ni kwa jinsi gani wanaume wengi tunasalitiwa na wapenzi wetu, msikilize kijana huyu ambaye ni mmoja wa waathirika wa tabia hii ya wasichana kujimilikisha wanaume zaidi ya mmoja.
Anasema: “Nilipobahatika kupata kazi nzuri nilijiapiza kuoa mke mzuri. Katika pitapita yangu nikakutana na binti mmoja mzuri sana ambaye tulianzisha uhusiano.
“Binti huyo alionesha kunipenda sana, majina ya baby, sweetie, honey ndiyo aliyokuwa akiyatumia kuniita, hata siku moja hajawahi kuniita jina langu.
“Kilichokuwa kinaniumiza kichwa ni kwamba, alikuwa na simu tatu na kila simu ilikuwa na laini mbili. Sikujua ni za nini namba zote hizo na zaidi ya yote, alikuwa hapendi niguse simu zake.
“Siku moja tukiwa chumbani kwangu, alibanwa na kifua. Alizidiwa na kuwa na hali mbaya iliyonilazimu nimkimbize hospitalini. Siku hiyo ndiyo nilijua uozo wake wote.”
Ushuhuda wa kaka huyu unatupa fundisho kubwa sana. Wasichana wengi wa mjini ni wazuri na wanayajua mapenzi kweli lakini wengi wao wametawaliwa na utapeli.
Itaendelea wiki ijayo...
globalpublishers
No comments:
Post a Comment