Kocha mkuu wa timu ya Young Africans Sports Club, Mholanzi Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Coastal Union katika mchezo wa mwisho wa kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom utakaofanyika siku ya jumapili katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz leo asubuhi katika mazoezi yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo anaamini mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.
Wachezaji wangu wapo fit wote, nadhani soka waliolicheza siku na Azam lilionekana, hizo ni dalili tosha kuwa wachezaji wanaelewa mafunzo yangu, hivyo naamin siku ya jumapili vijana wangu wataibuka na ushindi mzuri hali itakayotupelekea kuweza kuendelea kushika usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara amesema 'Brandts'
Coastal Union inayoshika nafasi ya nne katika msimo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, itashuka dimbani siku hiyo ya jumapili kusaka pointi ili kujiweka katika nafasi ya kuendelea kushika nafasi tatu za juu
Yanga ambayo mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa mabao 2 - 0 dhidi ya timu ya Azam FC katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki, itaingia uwanjani kusaka pointi 3 muhimu zitakazo ifanya iendelee kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwani kama Yanga ikishinda basi Simba na Azam hata zikishinda hazitoweza kuongoza Ligi.
Katika mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts ameendelea kufurahia kuwepo kwa wachezaji wake wote, kitu kitakachopelea kumtumia mchezaji yoyote atakayetaka kumtumia kwa mchezo huo wa jumapili, kwani hakuna mchezaji aliye majeruhi .
Vijana wa jangwani kwa sasa wanakamata nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kufikisha point 26, mbele ya Azam yenye pointi 24 na Simba yenye pointi 23 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 12.
No comments:
Post a Comment