
Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini asubuhi ya leo
Kikosi cha Young Africans kimefanya mazoezi leo asubuhi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ikiwa ni mazoezi ya mwisho kabla y akushuka dimbani kesho siku ya jumapili kucheza na wenyeji Coastal Union.
Young Africans ambayo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kufikisha jumla ya point 26 baada ya kushuka dimbani mara 12 na kushinda michezo 8, sare 2 na kufungwa 2, imetua jijini Tanga jana mchana ikiwa na kikosi kazi cha wachezaji 20.
Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema anashukuru kwa kufika salama jijini Tanga, na wachezaji wake wote wako fit na wamefanya mazoezi jana jioni katika Uwanja wa Gymkana na leo Mkwakwani hakuna mchezaji yoyote aliye majeruhi.
Aidha Brandst amesema kuwa anajua mchezo wa kesho utakua mgumu kwani vijana wake wanahitaji kumaliza mzunguko wa kwanza kwa ushindi ili hali Coastal Union wakitaka kushinda katika Uwanja wao wa nyumbani
Yanga ni timu bora, ina wachezaji bora katika Ligi ya Vodacom hivyo naamini wachezaji watacheza kwa nguvu na kuonyesha ufundi walioupata kutoka kwangu ili kupata ushindi na kudhihirisha ya kuwa Yanga ni timu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki alisema 'Brandts'
Mchezo huo wa kufunga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom utafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani kesho siku ya jumapili kuanzia majira ya saa 10 jioni.
No comments:
Post a Comment