ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 2, 2012

Alazimishwa kuishi na mume aliyemharibu kwa tindikali

BANGALADESH, India
WAKATI mwingine maisha ya ndoa hugeuka kuwa shubiri. Wapo watu wengi walioathirika katika maisha ya ndoa akiwamo Nurbanu.
Ingawa mpaka leo bado Nurbanu anaisha na makovu kutokana na ukatili aliofanyiwa na mumewe, lamelazimishwa kuendelea kuishi na mwanamume huyo, ambaye alimmwagia tindikali usoni baada ya kubaini kuwa, mumewe hakuwa mwaminifu.
Nurbanu anayeishi Bangaladesh, alipata majeraha hayo miaka 18 iliyopita baada ya kuolewa.
Nurbanu aliamua kutalikiana na mumewe baada ya kumfumania akiwa na mwanamke mwingine na suala hilo ndilo lililopelekea ukatili huo.
Siku nane baada ya talaka, alikuwa akipika nyumbani kwake, mumewe huyo alishuka katika pikipiki na kumwagia tindikali usoni na  alimwacha na upofu na majeraha yasiyopona.
Mumewe huyo ambaye kwa sasa ana miaka 36.
Nurbanu bado anaishi na mumewe huyo baada ya mama yake mzazi, kumlazimisha asaini hati ya kiapo na kumtoa mumewe gerezani kwa msamaha baada ya shambulio.
Mume wa Nurbanu alikuwa mafichoni kwa muda na aliendelea kutafutwa na mahakama kufuatia kosa hilo.   Lakini alikamatwa miezi kumi baadaye na kufungwa kwa miaka kadhaa kwa mujibu wa Shirika la Habari la The Huffington Post.
Mama yake alilipia fedha ya dhamana na kumtoa mwanawe kwa dhamana," alisema Nurbanu, ambaye alizaliwa katika maeneo ya Satkhira huko Kusini Magharibi mwa Bangaladesh.
"Alinilazimisha nitie saini ya kiapo ili atolewe. Aliwatumia watoto wangu kunisisitiza niolewe tena na baba yao." anasema.
"Watu watafikiri kuwa mume anamwangalia kwa ukaribu zaidi mkewe ambaye kwa sasa ni kipofu, lakini kitu kama hicho hakipo," anasema Nurbanu.
Anasema anadai kuwa,  mbali na kilema alichoachiwa, mpaka sasa mume wake anaendelea kumpiga na kumpa vitisho.
Anaongeza: "Hivi ndivyo maisha yangu yanavyosonga na sioni chochote ni maisha magumu sana."
Nurbanu, ambaye hawezi hata kuandaa chakula kwa ajili yake kutokana na ukatili aliowahi kufanyiwa na mumewe ni mmoja kati ya maelfu ya wanawake wanaokutana na ukatili wa kijinsia nchini India.
Monira Rahman, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Waathirika wa Tindikali (ASF), huko Bangaladesh amekuwa akifanya kazi na waathirika wa tindikali na petroli kwa muda wa miaka 14 sasa.
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, alisema kuwa idadi kubwa ya wasichana na wanawake wamekuwa wakipatamateso mikononi mwa watu ambao, wamekuwa wakiwachukulia kama bidhaa na kukiuka haki zao za kimsingi.
Rahman anasema kuwa idadi ya waathirika wa matukio ya aina hiyo jijini Bangaladesh imeshuka kutokana na msaada mkubwa kutoka serikalini, ambayo iomekuwa wakikemea vitendo hivyo pamoja na mashirika mbalimbali yaliyojitolea kwa kiasi kikubwa kutokomeza tatizo hilo.
Kulikuwa na matukio 111 ya shambulio la tindikali mjini Bangaladesh kwa mwaka 2011 ikilinganishwa na 500 ya mwaka 2002.
Lakini Rahma anasema  kwa kwa mwaka 2012 vurugu hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma, ambapo watu walikuwa wakishambuliwa mara kwa mara na hasa wanawake.
Kwa mujibu wa shirika la waathirika wa tindikali nchini India, jumla ya mashambulizi 59 tayari yameripotiwa nchini humo mwaka huu.
Kati ya waathirika 118 wa matukio hayo kwa mwaka 2011,  75 walikuwa wanawake na 13 wanaume,  wote wakiwa  na zaidi ya umri wa miaka 18.
Herieth Makwetta kwa msaada wa mtandao
Mwananchi

No comments: