Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad (39), anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa (16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika, Kwa picha zaidi wa tukio hilo bofya read more
Bwana Yussuf Hamad anatuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
Huyoooo anatoka nje ya mahakama
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
Njooni sasa huku kashika jiwe
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku akiwa na jiwe lake mkononi
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
Mkazi wa Mtaa wa Mbete. Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad (39), anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa (15) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi. Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo, lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.
Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka huu,
2 comments:
Kitu ambacho amefanya huyo Baba mzazi nichakinyama sana naninavyoona mimi huyo baba singe stahili kuwa nje kwa dhamana kosa alilotenda la jinai, hivi jamani hebu nifahamisheni ni kipengele gani cha sheria alicho kichukua hakimu huyu. naomba jibu ili haki itendeke
Ni kipengele kinachompa haki ya kujitetea kwa kila raia...tusisahau kuwa mtu afikishwapo mahakamani ni mtuhumiwa mpaka atakapopatikana na hatia... tabia ya kusweka watu rumande hovyo hovyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu: ( Lulu anasota rumande kwa ukatili wa mahakama na sheria mbovu zilizopo..:( Mnamkumbuka Ditopile wa Mzuzuri? Aliuwa mtu kwa bunduki lakini mahakama ilimpa mdhamana kwa kuwa alikuwa kigogo:( Tufunguke macho na mawazo pia waTanzania.. jela zimejaa wavuta bangi na watuhumiwa... mzigo kwa taifa kulisha watuhumiwa... ni watuhumiwa siyo wakosaji mpaka mahakama itakapo wahukumu tuache tabia tufuate mkondo wa sheria.
Post a Comment