WAKATI mabingwa wa Soka Bara, Simba wakikamilisha usajili wa mrithi wa kipa Juma Kaseja, Mganda Abbel Dhaira, mahasimu wao Yanga, wanatarajia kuwatoa kwa mkopo nyota wake wanane.
Dhaira amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola 40,000 (Sh43 milioni) na mshahara wa mwezi Sh2 milioni mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.
Kusajiliwa kwa kipa huyo kunakuja baada ya muda mrefu mashabiki wa Simba kuhoji kiwango cha Kipa Juma Kaseja.
Kaseja alikuwa gumzo kwa mashabiki wa Simba katika mechi za mwisho za duru la kwanza Ligi Kuu akituhumiwa kufungwa mabao ya kizembe.
Akizungumza jana baada ya kukamilika kwa usajili wa Dhaira, Hanspope alisema wanajivunia kupata kipa mwenye umbo kubwa kama Mohamed Mwameja aliyewahi kuidakia klabu hiyo.
Akizungumza jana baada ya kukamilika kwa usajili wa Dhaira, Hanspope alisema wanajivunia kupata kipa mwenye umbo kubwa kama Mohamed Mwameja aliyewahi kuidakia klabu hiyo.
Hanspope alisema kusajiliwa kwa kipa huyo Mganda kulitokana na mapendekezo kutoka kwa kipa wao wa kwanza hivi sasa, Kaseja.
“Kaseja ndiye aliyependekeza kwa uongozi kumsajili kipa huyu. Tunaamini mawazo yake yataisaidia Simba kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Dhaira alisema amefurahi kusajili Simba akiamini ni moja ya timu kubwa Afrika.
“Nimekuwa nikiisikia Smba kwa muda mrefu, nafahamu ni moja ya timu nzuri Ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla,” alisema kipa huyo.
Habari za uhakikia zilizonaswa na Mwananchi, zinadai kuwa wachezaji wanaojiandaa kuondoka Jangwani kwa mkopo ni Idrisa Rashid, Rashid Gumbo na Shamte Ally.
katika orodha hiyo, wengine ni Ibrahim Job, Salum Telela, Godfrey Taita, Omega Seme na Shaban Kado aliyerudishwa Mtibwa mzunguko wa kwanza.
katika orodha hiyo, wengine ni Ibrahim Job, Salum Telela, Godfrey Taita, Omega Seme na Shaban Kado aliyerudishwa Mtibwa mzunguko wa kwanza.
Hata hivyo chanzo hicho kimesema kuwa Kado alipelekwa Mtibwa kwa miezi sita na kwamba Coast Union wameonyesha kumuhitaji mzunguko wa pili Ligi Kuu.
“Mtibwa alikwenda kucheza kwa mkopo miezi sita, kuna mazungumzo yanaendelea lakini kwa asilimia kubwa atakwenda Union mzunguko wa pili,” alisema mtoa habari huyo.
Timu nyingine zilizoonyesha nia ya kumchukua kipa huyo ni African Lyon inayoshika mkia kwenye msimamo wa ligi Kagera Sugar, Coast na Mtibwa Sugar.
Timu nyingine zilizoonyesha nia ya kumchukua kipa huyo ni African Lyon inayoshika mkia kwenye msimamo wa ligi Kagera Sugar, Coast na Mtibwa Sugar.
“Tumeshakamilisha usajili wa Kabange Twite, hakuna mchezaji ambaye tutamuacha zaidi ya kuwapeleka kwa mkopo.”
Katibu mkuu wa Yanga Laurance Mwalusako alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo, alisema hakuna mpango wa kuacha wala kuongeza wachezaji zaidi ya Kabange Twite aliyesajiliwa hivi karibuni. Kabange ni ndugu na mchezaji Mbuyu Twite anayecheza Yanga.
Dirisha dogo la usajili kwa wachezaji wa nje linafungwa leo ,wakati kwa wachezaji wa ndani linatarajia kufungwa mwishoni mwa mwezi huu kwa mujibu wa TFF.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment