WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harisson Mwakyembe
WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harisson Mwakyembe amewataka Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari(TPA), wasioikubali bodi aliyoiteua hivi karibuni kuachia ngazi mara moja na kwamba watalipwa stahiki zao.
Akizungumza na wafanyakazi wa bandari hivi karibuni ambapo aliitambulisha bodi mpya ya TPA yenye wajumbe nane jijini Dar es salaam, Dk Mwakyembe alisema yeyote ambaye anahisi hataweza kufanya kazi na bodi hiyo anaweza kujiengua mwenyewe. Kuteuliwa kwa bodi hiyo kunatokana na kuvunjwa kwa bodi ya awali iliyobainika kutokuwa na ufanisi katika utendaji wa kazi jambo ambalo limesababisha TPA kukosa mapato huku wachache wakinufaika.
Mwakyembe alisema bodi hiyo itakuwa na wajumbe wanane na itaongozwa na Raphael Mollel, na amewataka wafanyakazi kuipa ushirikiano ili kutimiza malengo waliojiwekea.
“Bodi hii ni mpya naomba tuipe ushirikiano ili tuweze kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea,” alisema Dk Mwakyembe.
“Bodi hii ni mpya naomba tuipe ushirikiano ili tuweze kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea,” alisema Dk Mwakyembe.
Pia Mwakyembe aliwataka walioIngia kwa njia zisizo halali ikiwamo kuingizwa na ndugu zao wajiandae, kwani katika suala hilo hatakuwa na mchezo katika lengo la kuisafisha bandari.
“Nadhani wenyewe wanajitambua hivyo wajiandae, hatuko hapa kwa ajili ya kubebanabebana na matokeo yake ni ufanisi wa kazi kuwa mbovu na tutaanza kuwashughulikia siku chache zijazo,” alisema Dk Mwakyembe.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment