ILE Double Celebration ya kusheherekea uhuru wa Tanzania na Kenya iliyofanyika Luton Uingereza Jumamosi December 15, 2012 na kuaandaliwa na Luton Tanzanian Community kwa kushirikiana na Kenyan Community ilikuwa ya kufana na kupendeza, kulikuwa na ukataji keki ya Independence uliofanywanaMwenyekitiwa Luton Tanzanian Community Bw. John Mbwetekwakushirikiananakatibu wake Bw. Abraham Sangiwa. Mambo yalikuwa safi na palikuwa na burudani ya kila aina na genuine East African Cousine na vinywaji aina zote maana yake palikuwa hapatoshi. Umoja, amani, Upendo, Utani na Undugu ndivyo vilivyotawala katika shamrashamra hizi ambapo pia ndugu zetu wengi toka Uganda pia walijitokeza na kuahidi ushirikiano katika kudumisha Umoja wetu kama wana East Africa katika maeneo mbalimbali yanayotugusa pamoja.
Watanzania katika picha ya pamoja kwenye ile Double Celebration ya kusheherekea uhuru wa Tanzania na Kenya iliyofanyika Luton Uingereza Jumamosi December 15, 2012
Keki yenye bendera ya Tanzania ikikatwa katika ile Double Celebration ya kusheherekea uhuru wa Tanzania na Kenya iliyofanyika Luton Uingereza Jumamosi December 15, 2012 sherehe ziliandaliwa na Luton Tanzanian Community kwa kushirikiana na Kenyan Community
picha kwa hisani ya Abraham Sangiwa
………………………………………
Katibu Luton Tanzanian Community
No comments:
Post a Comment