ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 1, 2012

JB AKONGA NYOYO ZA MASHABIKI


Mwanamuziki nguli wa Kimataifa kutoka nchini DRC-Congo JB Mpiana akiimba  jukwaani mbele ya mashabiki kiduchu (hawapo pichani)  usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo kiingilio kilipangwa kuwa ni sh 25,000/= kwa laki moja wale wa VIP.
 Baadhi ya Wadau na mafundi wakiwa wamelizunguka Jenereta walipokuwa wakishindwa kubaini tatizo liko wapi kutokana na hitilafu zake za mara kwa mara.
 Mashabiki wakiserebuka hivyo hivyo mara JB Mpiana na kundi lake la Wenge BCBG walipopanda jukwaani.
 Baadhi ya Wanamuziki wa JB Mpiana wakitumbuiza jukwaani
 Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Mashujaa wakiongozwa na Chalz Baba wakitumbuiza jukwaani,kufuatia tatizo/hitilafu ya umeme bendi hiyo ilishindwa kuzinduza albamu yake ya Kidole Risasi.
 Mdau Ben Kinyaia kutoka Clouds TV akiruka Live kunasa matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
 Wadau waliofika kwenye uzinduzi wa albamu ya pili ya Mashujaa band
 H-Baba alitinga na mchuma huu lakini aliiishia kuutelekeza hapa kama uonekavyo.
 Pichani juu na chini ni madansa wa bendi ya Mashujaa wakitumbuiza jukwaani.


Copyright 2007 ©MICHUZI JR Picha kwa hisani ya Jiachie Blog

Mwanamuziki nguli wa Kimataifa kutoka nchini DRC-Congo JB Mpiana jana akiwa sambamba na wanamuziki wake wa bendi ya Wenge BCBG,usiku wa kuamkia leo walionesha unguli wao katika anga ya muziki wa dansi kwa kutumbuiza kwenye jukwaa la uzinduzi wa albamu ya pili ya bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Band iliyoitwa Risasi Kidole.

Aidha pamoja na JB Mpiana kutumbuiza mbele ya washabiki kiduchu waliofika kwenye uzinduzi huo haukufanyika kama ilivyotarajiwa na wengi,ilikuwa ni vituko uwanjani hapo,kwani kila wakati bendi ya Mashujaa ilipopanda jukwaani kwa ajili ya kutoa burudani,hitilafu za kile kilichodaiwa kuwa ni umeme zikawa kikwazo, hali hiyo ilipelekea bendi hiyo kushuka kabisa jukwaani mnamo majira ya saa nane kasoro hivi,huku wasanii wa utangulizi kushindwa kutumbuiza kabisa kwenye onesho hilo.

Baadaye ilielezwa kuwa jenereta lilikuwa na hitilafu,ambapo pia Mzee wa Jiachie alikuwapo eneo la tukio na kushuhudia mafundi wakivutana huku na kule kuhakikisha hali hiyo inatengamaa,lakini mnamo majira ya saa tisa kasoro hivi ikatangazwa JB Mpiana na skwadi lake watapanda jukwaani moja kwa moja,Maajabu ya Mussa walipopanda tu hakukutokea tena tatizo lolote la hitilafu ya umeme,baadae baadhi ya watu wakadai kwamba Ndumba Nangai ilitumika kuhakikisha bendi ya Mashujaa haizindui albamu yake kama ilivyotarajia.

Kama vile haitoshi baada ya hali kuwa tete kwenye viwanja vya lidaz usiku ule na ukiduchu wa watu,Mmiliki wa bendi ya Mashujaa atumbulikae kwa jina la Mama Sakina alishikwa na presha ya ghafla na Mzee wa Jiachie pia alishuhudia tukio hilo,ndipo wasamalia wema wakamkimbiza hospitali kupatiwa huduma ya kwanza,ambapo baadae hauikufahamika mapema alikimbizwa hospitali gani kwa matibabu.

No comments: