Rais Jakaya Kikwete, jana aliongoza mamia ya wananchi, viongozi mbalimbali wa serikali kutoka ndani na nje ya nchi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara, huku akijivunia amani, utulivu na maendeleo yaliyopatikana tangu kupatikana kwa uhuru.
Sherehe hizo zilikuwa na kauli mbiu isemayo 'Uwajibikaji, uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya taifa letu' pamoja na ujumbe usemao 'Uundaji Shirikishi wa Katiba mpya utadumisha amani nchini; toa maoni yako' zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kupambwa na vikundi vya ngoma za asili kutoka ndani na nje ya nchi.
Katika sherehe hizo, Rais Kikwete alitoa msamaha kwa wafungwa 3,814 huku wafungwa wa dawa za kulevya, rushwa, matumizi mabaya ya ofisi, wizi, kubaka na kulawiti wakikosa msamaha huo.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, ilisema msamaha huo utawahusu wafungwa wenye sifa mbalimbali.
Taarifa hiyo iliwataja wafungwa walionufaika na msamaha huo ni pamoja na wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi, ambao umri huo ni lazima uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Wengine ni wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili na ulemavu huo ni lazima nao uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba wengine ambao ni wafungwa wenye magonjwa kama Ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wako kwenye hatua ya mwisho ya ugonjwa ambao watathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Ilitaja wafungwa wengine ambao ni wa kike walioingia na mimba gerezani na walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonyesha ambao wote watanufaika na msamaha huo.
Kundi la mwisho la wafungwa wanaohusika na msamaha huo ni wafungwa wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano ambao hadi siku ya msamaha (jana), walikuwa wametumikia robo ya vifungo vyao.
Taarifa hiyo ilisema ni mategemeo ya serikali kwamba wafungwa waliopata msamaha huo watarejea katika jamii na kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa taifa na kuwaasa wajiepushe na kutenda makosa ili wasirejee gerezani.
Rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45 kifungu cha kwanza (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila, Rais wa Namibia Ifikepunye Pohamba, Waziri Mkuu wa Lesotho, Thomas Tabani, Makamu wa Rais wa Malawi, Khumbo Kachali na Makamu wa Rais wa Zambia, Dk. Guy Scott.
Wengine ni Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vincent, Waziri Mkuu wa Swatzland, Barnabas Lubisiso, Makamu wa Rais wa Visiwa vya Shelisheli, Daniel Faule, Waziri Mkuu wa Rwanda, Piere Damia, Waziri wa Mambo ya Nje ya Zimbabwe, Simba Rasha, Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) na viongozi wengine kutoka nje na ndani ya nchi.
Viongozi wengine ni waandamizi na wastaafu wa serikali ambao ni Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, viongozi wengi wa serikali pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.
Rais Kikwete aliwasili uwanjani hapo saa 4:00 asubuhi akiwa katika gari la wazi na muda mfupi baadaye, alipigiwa mizinga 21 ikiwa ni heshima kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Baadaye, Rais Kikwete alikagua gwaride rasmi la maadhimisho hayo kisha gwaride hilo lililoundwa na askari kutoka majeshi ya ulinzi na usalama likiongozwa na Kamanda Fadhili Omary Nyondo, lilipita mbele yake na kutoa heshima kwa mwendo wa pole na haraka.
Pia sherehe hizo zilipambwa na vikundi vya halaiki vyenye watoto 2,625 kutoka bara na visiwani, maonyesho ya sura ya kitabu yaliyofanywa na watoto 1,440 wakiongozwa na Athumani Kambwagwa, kikundi cha ngoma cha Nyota kutoka Dodoma, kikundi cha taifa Zanzibar, kikundi cha ngoma cha utandawazi kutoka Ukerewe mkoani Mwanza pamoja na kikundi cha ngoma cha Taifa cha Rwanda.
Katika mazungumzo yake mafupi aliyoyatoa kwa umma, Rais Kikwete aliwapongeza Watanzania kwa kutimiza miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara huku wakiendelea kudumisha amani na utulivu na mafanikio tele katika nyanja mbalimbali.
Alisema tangu Tanganyika ipate uhuru, mafanikio mengi yamepatikana katika nyanja za elimu na miundombinu.
Kivutio kikubwa katika maadhimisho hayo ambacho kiliwainua viongozi mbalimbali kwenye viti ni ngoma ya kikundi cha Utandawazi kutoka Ukerewe ambayo ilichezwa kwa umahiri na mvuto na watoto wadogo wenye umri wa miaka mitatu kitendo ambacho kiliwavutia viongozi na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Kwa upande wake, Rais wa Namibia, Ifikepunye Pohamba, aliwapongeza Watanzania kwa mafanikio ya kutimiza miaka 51.
Alisema siku hiyo ambayo Tanzania bara inapata uhuru, yeye na viongozi wengine kutoka Namibia walikwapo katika Uwanja wa Uhuru kushuhudia sherehe hizo.
“Ninajisikia furaha kujumuika nanyi tena leo tangu mlipopata uhuru, nakumbuka siku hiyo nilikuja jijini Dar es Salaam na pia nilikwenda Dodoma, nimefurahi sana kushiriki kwa mara ya pili,” alisema Pohamba.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment