Tunaukaribisha
mwaka 2013 kwa kuwaletea ubao mpya wa malumbano ya hoja:
Filosofa Forum (www.filisofaforum.com)
Katika fani hii
ya mawasiliano, iwe kwa blog za jamii, barua pepe, magazeti, tovuti na aina
nyingine nyingi, jambo moja ambalo baadhi yetu wadau wa malumbano ya hoja
tungependa kuweka juhudi kulibadilisha katika mwaka huu mpya 2013, ni jukwaa la
habari, mipasho (malumbano) ya kisiasa, kimichezo, na utani wa kikabila, wenye
ustaarabu na maadili yaliyopevuka bila kudhihaki jinsia, dini, maumbile au
kabila la mtanzania yeyote. Awe mtoto, kijana, mzee, mvulana, msichana,
mwanaume au mwanamke, Filosofa Forum
inaamini sisi sote ni matokeo ya uumbaji wa mwenyezi mungu.
Hivyo
basi kama unaamini kwa dhati kuwa huu
ndo mwelekeo unaostahili katika malumbano ya hoja bila vioja, hapa ndio mahali
muafaka ambapo mijadala ya aina zote itazingatia maadili , uwazi, na kuheshimu
tofauti za kiitikadi, dini , na tamaduni zote za mtanzania.
KARIBUNI SANA UELIMIKE NA KUELIMISHA WENGINE
Happy
New Year 2013
By
Filosofa Forum team.
No comments:
Post a Comment